MAKUBALIANO YA KUANZISHA NDEGE YA MOJA KWA MOJA KUTOKA TANZANIA HADI DALLAS KUKUZA SEKTA YA UTALII.

MAKUBALIANO YA KUANZISHA NDEGE YA MOJA KWA MOJA KUTOKA TANZANIA HADI DALLAS KUKUZA SEKTA YA UTALII.

Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani  zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji   pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii.  Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya vikao vya

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe alioambatana nao wakipewa maelezo kutoka kwa Mark Davidson ( wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili katika  Bodi ya Utalii ya Dallas ambapo wamefanya ziara ya  kutembelea katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza namna Bodi hiyo inavyofanya kazi zake katika kutangaza  utalii .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA,Brigedia Jenerali ( Hamisi Semfuko)  akiwa na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Dkt. Elsie Kanza ( wa kwaza kulia)  wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendahji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo yao wamekubaliana  kuimarisha ushirkiano  katika uhifadhi wa wanyamapori.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa nne kulia)   akiwa na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani  n  Dkt. Elsie Kanza (katikati)  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA,Brigedia Jenerali  Hamisi Semfuko ( wa nne kushoto)  wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Makumbusho ya aliyekuwa Rais wa Marekani, John Kennedy. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe alioambatana nao na Makamu wa Rais wa Utalii wa Dallas  Balozi Mhe. Mark Thompson (wa tano kushoto ) mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo wamekubaliana kuanzisha ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Marekani katika Jimbo la Dallas. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza na wa nne  kulia ni Brigedia Jenereli, Hamisi Semfuko

Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani  zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji   pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii.

 
Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya vikao vya ana kwa nyakati tofauti  kwa lengo la kujifunza namna wanavyoendesha shughuli za utalii pamoja kukuza ushirikiano baina ya pande zote mbili.

 
“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Jimbo la Dallas  pamoja na kuangalia namna tunavyoweza kuliteka soko la watalii katika Jimbo hilo, tumejadili mikakati ya kuanza na watalii ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu katika jimbo hilo lengo likiwa ni kupata soko la uhakika la  watalii wengi zaidi katika  siku za usoni ” Amesema Waziri Ndumbaro.


Akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Jimbo la Dallas Liliana Rivera, Dkt. Ndumbaro amesema moja ya shabaha kubwa ni kuhakikisha kunaanzishwa  ndege ya moja kwa moja ya kutoka Tanzani kwenda Dallas ambapo amesema itaweza kusaidia  Watanzania ambao ni watalii kwenda Dallas na Watalii kutoka Dallas kutembelea Tanzania.


” Tanzania imeshaanzxa mazungumzo na Uongozi wa Jimbo hilo ili kuhakikisha hilo linafanikiwa na hivi wiki lijalo Mkurugenzi wa Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) atakuja Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzio hayo.


Katika ziara hiyo pia,   Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mchezo wa Gofu nchini Marekani, Bruce Davidson ambapo Dkt.Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuinadi Tanzania kuwa  ipo  tayari kuwa  Mwenyeji wa mashindano makubwa  ya mchezo wa gofu yatayohusishwa Wachezaji mahiri wa mchezo huo .


Aidha, Katika mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro wamekubaliana kutangaza vivutio vya utalii kupitia mchezo huo kwa kutumia vyombo vya habari vya kimataifa vitakavyotumiwa katika kutangaza mchezom huo.


Katika hatua nyingine, Waziri Ndumbaro  amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo hayo wamezungumza maeneo ya kushirikiana ikiwemo kukuza utalii wa uwindaji na kutoa vifaa vya kukabiliana na  ujangili wa wanyamapori.


Aidha, Katika mazungumzo hayo wamejadiliana  masuala ya Uwekezaji  ambapo Dkt.Ndumbaro amewaita Wawekezaji wa Marekani hususan Matajiri wa Jimbo la Dallas kuja kuwekeza Tanzani kwa kujenga mahoteli yenye hadhi ya nyota tano.


Katika vikao hivyo vya Waziri Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  nchini Marerkani  Dkt. Elsie Kanza pamoja na Ujumbe wa kutoka Tanzania akwemo Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jenerali, Hamisi Semfuko, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi na Afisa Mwandamizi, Segoline Tarimo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »