BREAKING: Channeli za bure zarudishwa DSTV, Waziri Nape atangaza rasmi

BREAKING: Channeli za bure zarudishwa DSTV, Waziri Nape atangaza rasmi

Waziri wa Habari Nape Nnauye leo ametangaza rasmi kurudishwa kwa TV channels za bure kwenye king’amuzi cha DSTV mfano CloudsTV, ITV n.k baada ya kutembelea ofisi za Multichoice Tanzania (DStv) Dar es salaam. “Moja ya maagizo ya Mh. Rais Samia ni kuboresha mawasiliano, sasa katika maboresho tunazo baadhi ya kanuni, sera na sheria ambazo inabidi

Waziri wa Habari Nape Nnauye leo ametangaza rasmi kurudishwa kwa TV channels za bure kwenye king’amuzi cha DSTV mfano CloudsTV, ITV n.k baada ya kutembelea ofisi za Multichoice Tanzania (DStv) Dar es salaam.

“Moja ya maagizo ya Mh. Rais Samia ni kuboresha mawasiliano, sasa katika maboresho tunazo baadhi ya kanuni, sera na sheria ambazo inabidi tuwe tunazibadili mara kwa mara ziendane na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani” — Nape.

“Leo pamoja na kuwashukuru DSTV Tanzania kwa kazi nzuri mliyofanya na kutambua mchango wenu kwenye sekta yetu nikasema leo nitangaze moja ya mabadiliko tuliyoyafanya kwenye kanuni zetu, kuna kanuni namba 18 ya mwaka 2018 inayohusiana na miundombinu ya utangazaji wa kidigitali, tumeifanyia marekebisho ili kuruhusu Channel za TV ambazo hazilipiwi (mfano CloudsTV, ITV n.k) ziweze kuonekana kwenye king’amuzi cha DSTV” — Nape.

1 comment
Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

1 Comment

  • Alex Cyprian
    January 31, 2022, 9:44 am

    Excellent Nape

    REPLY

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »