Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega amesema serikali imeanza hatua za utoaji elimu ya ufugaji kwa wanafunzi kwa kuanzisha Club zitakazowajengea uwezo wa ufugaji na kuwapatia ajira hata baada ya kumaliza masomo yao. Amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kukusanyia na kusindika bidhaa za maziwa kwa vyama
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Ulega amesema serikali imeanza hatua za utoaji elimu ya ufugaji kwa wanafunzi kwa kuanzisha Club zitakazowajengea uwezo wa ufugaji na kuwapatia ajira hata baada ya kumaliza masomo yao.
Amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya kukusanyia na kusindika bidhaa za maziwa kwa vyama vya ushirika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Alisema Club hizo za kutoa elimu ya ufugaji wa aina mbalimbali za mifugo zitaanzishwa hasa kwenye shule zenye maeneo makubwa ili wanafunzi wapate eneo la kutosha kwa ufugaji
Mheshimiwa Ulega alisema madarasa hayo kwa wanafunzi shuleni yataanzishwa katika mikoa ambayo wananchi wake hawana kabisa ujuzi wa ufugaji sambamba na ujuzi wa usindikaji wa maziwa.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *