Msemaji Mkuu wa Serikali: Filamu ya Royal Tour hazikutumika fedha za Watanzania

Msemaji Mkuu wa Serikali: Filamu ya Royal Tour hazikutumika fedha za Watanzania

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amefanya mahojiano na Wasafi TV na hii ni sehemu ya nukuu zake kuhusu filamu ya Royal Tour ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Aprili 18, 2022 Nchini Marekani: Sababu za Wamarekani kupewa tenda“Ile filamu uzinduzi wake ni Tarehe Aprili 18 na utafanyika mara mbili New York na Los Angels, sasa mnauliza kwa

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amefanya mahojiano na Wasafi TV na hii ni sehemu ya nukuu zake kuhusu filamu ya Royal Tour ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Aprili 18, 2022 Nchini Marekani:

Sababu za Wamarekani kupewa tenda
“Ile filamu uzinduzi wake ni Tarehe Aprili 18 na utafanyika mara mbili New York na Los Angels, sasa mnauliza kwa nini walirekodi wageni na si Watanzania? Unachokifanya lazima uwe na malengo.

“Sisi malengo yetu kwenye filamu hii ni kuifikia dunia na kuiambia fursa zetu za utalii na uwekezaji na biashara, sasa rafiki yangu Ukimchukua Msigwa aende akarekodi hiyo filamu si ataishia kutazama Zungu na nyie Wasafi mtanisifia tu lakini vipi kwenye kuwafikia walengwa?”

Lengo ni wasanii milioni 5 kwa mwaka
“Waliotengeneza filamu wanaenda kuizundulia Marekani, maana yake kule tayari unaanza kuwafikia watu wengi ambao ni walengwa. Tunataka watalii wafike milioni 5 kwa mwaka ikifika mwaka 2025.

“Idadi ya watalii ilishuka mpaka chini ya laki 6 kutokana na Corona.

“Ripoti ya safari hii inaonesha tumeshafikia watalii milioni 1.7 na tunataka tuendeleze hiyo kasi na tunataka pia watu maarufu duniani ambao hawakai Bombambili au Njombe, wako Los Angeles, Newyork, London huko

Hazikutumika fedha za Watanzania
“Tutapata watalii ili tupate fedha za kujenga shule, vituo vya afya na barabara na mahitaji mengine. Gharama alishazisema Mhe. Rais lakini watu wajue tu kuwa hatukutumia fedha za Watanzania. Kwanza wanaoandaa kipindi wana sera yao ya kutotumia fedha za serikali.

“Watanzania tushabikie hii filamu na tunahitaji kumpongeza sana Mhe. Rais katika hili. Miaka ya nyuma tulitaka kufikisha utalii kwenye majukwaa ya kimataifa tukaletewa bili ya mabilioni tukakimbiana.”



============================

Mwezi uliopita Rais Samia Suluhu Hassan alinukuliwa akisema hivi: “Tulifanya kuchangisha fedha nadhani tulichangisha kiasi cha bilioni 11 ambazo mpaka tunamaliza shooting (Royal Tour) na kila kitu, tulitumia kama bilioni 7 gharama za kila kitu. Haikutoka fedha serikalini ile yote ilikuwa ni kuchangisha mashirika.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »