RAIS SAMIA AZINDUA ‘THE ROYAL TOUR’ NCHINI MAREKANI (PICHA +VIDEO)

RAIS SAMIA AZINDUA ‘THE ROYAL TOUR’ NCHINI MAREKANI (PICHA +VIDEO)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Guggenheim Museum, New York nchini Marekani. FILAMU ya The Royal Tour imezinduliwa katika ukumbi wa Guggenheim Museum Jijini New York nchini Marekani kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia leo ambapo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Guggenheim Museum, New York nchini Marekani.

FILAMU ya The Royal Tour imezinduliwa katika ukumbi wa Guggenheim Museum Jijini New York nchini Marekani kwa mara ya kwanza usiku wa kuamkia leo ambapo Rais Samia alihudhuria uzinduzi huo.

Katika uzinduzi huo Rais Samia alipata wasaa wa kuhojiwa ambapo alitumia fursa hiyo kuielezea Tanzania kwa uzuri wake na kuwaasa raia wa Marekani na dunia kwa ujumla kwenda Tanzania kufanya utalii kwani hawatajutia.

Moja ya jambo ambalo liliwavutia wengi ni pale rais Samia alipotanabaisha kuwa kitendo cha yeye kuendesha gari kwenye utengenezaji wa filamu hiyo ilikuwa ni cha mara kwanza baada ya miaka 15.

Wakati akirekodi filamu hiyo pamoja na mwongozaji maarufu wa filamu, Peter Greenberg, Rais Samia alitembelea na kuonyesha kwa wageni vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.

Katika Mahojiano hayo Rais Samia amewaelezea watanzania kama watu wakarimu na rafiki kwa kila mtu pia ameelezea kuwa nyakati nzuri kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii ni mwezi Juni na Agosti kipindi ambacho hakuna mvua wala hakuna joto, kwa wale ambao wanatamani kuona makundi ya wanyama yakiwa yanahama ingawa watalii wanaweza kuja muda wowote watao nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitazama Filamu ya Royal Tour pamoja na Wageni mbalimbali mashuhuri New York nchini Marekani.

Rais Samia pia ameelezea jitihada ambazo zinafanywa na Serikali ya Tanzania za kuwahamasisha waigizaji wa kike na wa kiume katika kutumia vipaji vyao na Sanaa kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii akidai kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na nchi 5 zinazoongoza kwa utalii nchini Tanzania na kwamba wamekubaliana kuchukua hatua madhubuti katika kusaidia kuinua sekta ya utalii nchini Tanzania.

Muandaaji wa filamu hiyo Peter Greenberg amesema uzinduzi wa filamu hiyo utaendelea katika maeneo mengine nchini Marekani ambapo Rais Samia anatarajiwa kwenda jijini Los Angeles kwa ajili ya shughuli hiyo.

Rais Samia, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mwandaaji wa filamu ya Royal Tour na Baadhi ya Wafanya Biashara wa Nchini Marekani baada ya Futari Jijini New York Marekani

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »