JIJI LA DODOMA KUFANYA UHAKIKI MADHUBUTI KATIKA KUHAMISHA WAFANYABIASHARA SABASABA ILI KILA MFANYABIASHARA ANAPATE STAHIKI YAKE.

JIJI LA DODOMA KUFANYA UHAKIKI MADHUBUTI KATIKA KUHAMISHA WAFANYABIASHARA  SABASABA ILI KILA MFANYABIASHARA ANAPATE  STAHIKI YAKE.

Na.Faustine Galafoni,Dodoma, Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema katika zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo[Machinga]katika soko la Sabasaba ili kupisha ujenzi na ukarabati wa soko hilo lazima uhakiki madhubuti ufanyike ili kila mfanyabiashara apate haki yake . Mafuru amebainisha hay oleo April,20,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na baadhi ya

Na.Faustine Galafoni,Dodoma,

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema katika zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo[Machinga]katika soko la Sabasaba ili kupisha ujenzi na ukarabati wa soko hilo lazima uhakiki madhubuti ufanyike ili kila mfanyabiashara apate haki yake .

Mafuru amebainisha hay oleo April,20,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na baadhi ya wafanyabiashara katika soko la sabasaba kuendelea kuwa na wasiwasi juu ya panguapangua ya wafanyabiashara katika soko la sabasaba kupisha ujenzi.

Hivyo,Mafuru amefafanua kuwa lengo la jiji ni kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na si kuwadhurumu.

Aidha,Mkurugenzi huyo wa jiji la Dodoma amesema wapangaji waliojimilikisha Zaidi ya kibanda kimoja watamiliki kibanda kimoja tu ili kuwapa nafasi watu wengine kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara wamejimilikisha Zaidi ya vibanda 20 na kuvipangisha kwa watu wengine kwa bei ya juu.

Afisa biashara jiji la Dodoma Donatila Vedasto amesema lengo la  kuwahamisha kwa muda wafanyabiashara ni kupisha uboreshaji wa miundombinu huku mwekahazina wa jiji  Rahabu Philiph akisema mpango wa ukarabati wa soko la sabasaba ni wa kitambo lakini haukutekelezwa kwa wakati kutokana na ufinyu wa bajeti uliokuwepo.

Ikumbukwe kuwa Katika mkakati wa uboreshaji wa soko la sabasaba Machi,4,2022  mkuu wa mkoa  wa Dodoma Anthony Mtaka aliliagiza jiji la Dodoma kuwaorodhesha wafanyabiasha wote katika mfumo maalum ili kuweza kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza hapo baadaye ambapo mkakati   wa jiji ni ujenzi wa soko  jipya sabasaba litakaloweza kuhudumia Zaidi ya wafanyabiashara elfu saba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »