RAIS MWINYI AMEKUTANA NA UJUMBE WA IMF

RAIS MWINYI AMEKUTANA NA UJUMBE WA IMF

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. HusseinAli Mwinyi amelipongeza Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwakuendelea kuinga mkono Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake.Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar wakati alipokutana nakufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), ukiongozwana Mshauri wa Shirika hilo wa masuala ya maendeleo Barani

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein
Ali Mwinyi amelipongeza Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwa
kuendelea kuinga mkono Zanzibar katika kuimarisha uchumi wake.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar wakati alipokutana na
kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), ukiongozwa
na Mshauri wa Shirika hilo wa masuala ya maendeleo Barani Afrika Charalambos
Tsangarides.
Katika maelezo hayo Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Shirika la (IMF) limekuwa ni
msaada mkubwa kwa Zanzibar kutokana na juhudi zake inazoendelea kuzichukua
katika kuiunga mkono Zanzibar hasa katika kipindi hichi ambacho uchumi wa
dunia umedorora.
Alieleza kuwa mkopo fedha za Uviko-19 zilizotolewa na Shirika hilo kwa Zanzibar
ulikuwa na umuhimu mkubwa na kuweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika
maendeleo ya Zanzibar katika kipindi ambacho uchumi wake ulitetereka
kutokana na janga la maradhi hayo.
Aliongeza kuwa hatua hiyo inafaa kupongezwa kwani ilisaidia kwa kiasi kikubwa
kutokana na wakati ambapo sekta ya utalii ambayo imekuwa na mchango
mkubwa katika uchumi wa Zanzibar iliathirika kutokana na janga la Uviko- 19.
Alifahamisha kwamba kuathirika kwa sekta ya utalii ilipelekea kuiathiri sana
bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na sekta hiyo kuwa ndiyo
muhimili mkuu wa uchumi ambayo ina mchango mkubwa katika bajeti pamoja
na pato la Taifa.
Rais Dk. Mwinyi aliueleza ujumbe huo kwamba mkopo huo wa Uviko-19
uliotolewa na (IMF) uliweza kuchangamsha uchumi wa Zanzibar ikiwa ni pamoja
na kuimarisha ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
Alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika hilo la Fedha Duniani (IMF), pamoja na
timu hiyo iliyofika Zanzibar kwa azma yake ya kuendelea kuisaidia Zanzibar
katika awamu ya pili ambapo fedha zitakazopatikana katika mkopo huo zitalenga

2

kuendeleza yale yote yaliyoanzwa katika mkopo wa awali ikiwemo ujenzi wa
miradi ya maendeleo.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa fedha hizo pia, zitasaidia katika kufufua
uchumi kwa kuzingatia maeneo ya vipaumbele vya Serikali pamoja na
kuwajengea uwezo wafanyakazi hasa katika maeneo ya masuala ya bajeti
pamoja na takwimu.
Nae Mshauri wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), katika masuala ya maendeleo
Barani Afrika Charalambos Tsangarides alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk.
Mwinyi pamoja na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuutumia
vyema mkopo huo.
Katika mazungumzo hayo, Mshauri huyo wa Shirika la (IMF), wa masuala ya
maendeleo Barani Afrika alieleza kuridhika kwake na juhudi zilizochukuliwa na
Zanzibar katika kuhakikisha mkopo uliotolewa na Shirika hilo unatekeleza vyema
shughuli zilizokusudiwa.
Bwana Tsangarides alimueleza Rais Dk. Mwinyi jinsi Shirika hilo lilivyopata hamu
ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuongeza
awamu ya pili ya fedha za mkopo ambazo zitasaidia kuendeleza miradi ya
maendeleo sambamba na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Pamoja na hayo, Mshauri huyo alieleza hatua mbali mbali zitakazochukuliwa na
(IMF) katika kuhakikisha Zanzibar inafaidika moja kwa moja na fedha hizo ili
kuweza kurahisisha shughuli zake za kiuchumi na kimaendeleo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »