RAIS MWINYI ATANGAZA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA 15%

RAIS MWINYI ATANGAZA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA 15%

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali itaongeza mshahara kwa kutumia utaratibu wa kuwapanga watumishi katika madaraja na vyeo kwa mujibu wa miundo ya utumishi kwa kuzingatia elimu zao pamoja na uzoefu wa kazi. Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo huko katika

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali itaongeza mshahara kwa kutumia utaratibu wa kuwapanga watumishi katika madaraja na vyeo kwa mujibu wa miundo ya utumishi kwa kuzingatia elimu zao pamoja na uzoefu wa kazi.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya Maisara kwenye hotuba yake aliyoitoa ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi), ambapo kwa Zanzibar sherehe hizi zimefanyika hivi leo, hii ni kufuatia kuwapa wananchi wa Zanzibar muda wa matayarisho ya skukuu ya Idd el Fitr.

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa ana imani kwamba ongezeko la mishahara litakalofanywa litakuwa na mchango katika kuimarisha uwezo wa watumishi wa umma kujikimu kimaisha pamoja na kuondoa kilio cha muda mrefu kwa watumishi wa umma ambapo elimu na uzoefu wao wa kazi haukuwa ukijitokeza wazi wazi katika marekebisho ya mshahara yaliyofanywa vipindi vilivyopita.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alsiema kwua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga TZS bilioni 12.7 kwa mwezi sawa na TZS bilioni 153 kwa mwaka kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa zoezi hilo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Alisema kuwa kutokana na utaratibu huo mshahara wa kima cha chini kwa mtumishi aliyeajiriwa mwaka 2019 utapanda kutoka 300,000/ hadi kufikia TZS 347,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.6.

Aliongeza kwua vile vile kwa mtumishi wa elimu ya ngazi ya cheti wka masomo ya Art aliyeajiriwa katika mwaka huo huo mshahara wake utapanda kutoka TZS 321,000 hadi kufikia TZS 382,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.

Kwa maana hiyo, Rais Dk. Miwnyi alisema kwamba kila mfanyakazi atapara nyongeza ya mshahara kutegemea na elimu yake pamoja na muda aliofanya kazi ambapo mfano huo ni kwa mfanyakazi mpya hivyo hata ambae hana cheti lakini amefanya kazi muda mrefu mshahara wake utaongezeka kwa kadri ya muda aliofanyakazi.

Vile vile, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa katika kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanaendelea kuwa na kipato hata wanapopata changamoto ya kupoteza ajira au kupata ajali wakiwa kazini, Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) imeanzisha Fao la Upotevu wa Ajira na Fao la Kuumia Kazini.

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa mafao hayo yataanza kutolewa kuanzia mwaka wa fedha ujao ambapo hivi sasa kazi ya kukamilisha taratibu za kisera na kisheria zinaendelea vizuri na ziko katika hatua za mwinsho kukamilika.

“Kwa mara nyengine nawanahisi watumishi wa umma kwamba, Serikali itaendelea kuimarisha maslahi ya watumishi wa umma kadri ya hali ya uchumi itakavyoruhusu”, alisema Rais Dk. Mwinyi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuanzisha Bima ya Afya katika mwaka ujao wa fedha ambapo itaanza kwa wafanyakazi wa Serikali kisha yataingizwa makundi mengine lengo ni kuwa na Bima ya Afya kwa wananchi wote wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa maelezo ya Rais Dk. Mwinyi tayari Serikali imelipa jumla ya TZS Bilioni 1.8 kwa madeni ya wafanyakazi wa Serikali ikiwa ni pamoja na TZS Bilioni 4.9 za wazabuni.

Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba katika mwaka wa fedha ujao Serikali itaajiri Watumishi wapya 5,639 katika sekta mbali mbali za Utumishi wa Umma ikwiemo Afya, elimu pamoja na sekta nyengie ili kuweza kutekeleza azma hiyo Serikali imetenga jumla ya TZS bilioni 24.6 katika bajeti ya mwaka ujao kwa ajili ya kugharamia ajira hizo mpya.

Dk. Mwinyi alikemea tabia ya baadhi ya viongozi ambao alisema wamefilisika kiuongozi kwa kutoa visingizio visivyo vya ukweli katika kuwapa wafanyakazi haki zao kwa kusingizia kwamba wamepewa maagizo na Rais na kusema kwamba kiongozi yeyote atakae tumia lugha hiyo atawajibishwa.

Nae Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhan  Soraga alieleza Afisi yake shughuli zilizofanywa na Afisi yake ikiwa ni pamoja na kuunda Bodi, kutoa elimu na kufanya ukaguzi maalum wa kufuatilia ulipwaji wa kima cha chini cha mshahara kilichotangazwa na Serikali ambapo taasisi 213 zililipa ipasavyo mbapo taasisi 19 hazikutii sheria.

Akitoa salamu zake Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki Bwana Werllingtoa Chibebe alitoa pongezi kwa Rais Dk. Mwinyi kutokana na mafanikio ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni ambayo Serikali anayoiongoza inaendelea kuyatekeleza sambamba na juhudi zinazoendelea katika kupambana na Uviko-19.

Alisema kuwa ILO inathibitisha uungaji mkono na ushirikiano wake na Serikali, vyama vya wafanyakazi na waajiri pamoja na wadau wengine na kutoa wito kwa wadau wote na kusisitiza haja ya kuunganisha nguvu ili kujenga mazingira  ya kazi yanayozingatia haki na utu.

Mapema akisoma risala ya wafanyakazi kupitia shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC), Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Khamis Mwinyi Mohammed aliipongeza Serikali na uongozi wa Awamu ya Nane kwa hamu iliyonayo ya kutaka kuona nchi inapata maendeleo.

Katika risala yake hiyo Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa kima cha chini cha mshahara hivi sasa ni TZS 300,000 kiwango ambacho pia, kinakatwa Kodi na mikato mingine ya kisheria, hivyo basi kinachobaki mkononi hakimkidhi mfanyakazi hata kwa robo ya mwezi.

Hata hivyo, aliwaomba wasaidizi wa Rais kubadilika na wajali thamani ya mazungumzo katika kuhimiza wajibu na maslahi ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kueleza changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Serikali.

Alieleza jinsi maslahi ya baadhi ya wafanyakazi katika baadhi ya Wizara  yanavyopata changamoto ikiwa ni pamoja na marekebisho yaliyovuruga Kikokotoo cha mafao ya uzeeni ambayo miongoni mwa changamoto zake ni kupungua kwa kiinua mgongo.

Sambamba na hayo, alieleza tabia iliyojengeka kwa watendaji kufanya mambo yasiyofaa kwa kisingizio cha ‘Rais kasema’ ambapo baadhi ya mambo hayo ni kutolipa haki na madai halali ya wafanyakazi pamoja na kuwadhalilisha.

Akitoa neno la ukaribisho Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa alieleza jinsi wananchi walivyofarajika na juhudi za Rais Dk. Mwinyi katika kuwaletea maendeleo endelevu.

Rais Dk. Mwinyi alitoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa mwaka huu pamoja na kutoa vikombe kwa washindi wa mashindano ya mpira wa miguu yaliyofanyika ambapo mapema mara tu baada ya kufika viwanjani hapo aliyapokea maandamano ya wafanyakazi mbali mbali kutoa sekta ya umma na sekta binafsi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »