FORM FIVE SELECTION/ JINSI YA KUPATA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2022

FORM FIVE SELECTION/ JINSI YA KUPATA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO 2022

Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amesema jumla ya wanafunzi 153,219 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu na elimu ya ufundi kwa mwaka 2022. Kati ya hao, wanafunzi wa 90,825 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mpya 22 za Serikali. Huku akibainisha kuwa kati yao wenye mahitaji maalumu 481. “Wanafunzi

Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amesema jumla ya wanafunzi 153,219 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ualimu na elimu ya ufundi kwa mwaka 2022.

Kati ya hao, wanafunzi wa 90,825 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mpya 22 za Serikali. Huku akibainisha kuwa kati yao wenye mahitaji maalumu 481.

“Wanafunzi 41,401 wakiwemo wasichana 17,390 watajiunga kusoma tahususi za sayansina hisabati. Huku wanafunzi 47,133 wakiwemo wasichana 25,508 watajiunga kusoma tahasusi za masomo ya Sanaa, lugha na biashara,” amesema Bashungwa.

Waziri huyo ameeleza hayo leo Alhamisi Mei 12, 2022 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na elimu ya ufundi, akisema wanafunzi hao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu wametoka katika shule za Serikali na binafsi.

Bashungwa amefafanua kuwa kati ya wanafunzi 153,219 wasichana 67,751 na wavulana  85,678 sawa na asilimia 91.8 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo elimu ya ufundi kwa mwaka huu.

“Muhula utaanza Juni 13 mwaka huu, wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na kidato cha tano wanapaswa kuanza kuripoti katika shule walizopangiwa. Juni 30 itakuwa siku ya mwisho ya kuripoti kwa wanafunzi.ADVERTISEMENT

“Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti, nafasi itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.Uchaguzi wa shule na vyuo umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule,” amesema Bashungwa.

Kwa mujibu wa Bashungwa, wanafunzi 14,254 wakiwemo wasichana 3,901 na wavulana 10,353 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka huu.

Hii hapa Link ya kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga kitado cha Tano kwa Kila Mkoa

https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »