Waziri wa nchi Mhe. Mudrick amekagua ujenzi wa kituo cha kuchakata asali.

Waziri wa nchi Mhe. Mudrick amekagua ujenzi wa kituo cha kuchakata asali.

Wajasiriamali wanajishughulisha na uzalishaji wa asali nchini wametakiwa kuvitumia vituovinavyojengwa na serikali kwa ajili ya kuendesha shuguli zao kwa ufanisi na kujipatia masoko ya uhakika. Ameyasema hayo na Waziri wa nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick RamadhanSoraga wakati wa kukagua hatua za ujenzi wa kituo cha kuchakata mazao ya asali kinachojengwa

Wajasiriamali wanajishughulisha na uzalishaji wa asali nchini wametakiwa kuvitumia vituo
vinavyojengwa na serikali kwa ajili ya kuendesha shuguli zao kwa ufanisi na kujipatia masoko ya uhakika.


Ameyasema hayo na Waziri wa nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramadhan
Soraga wakati wa kukagua hatua za ujenzi wa kituo cha kuchakata mazao ya asali kinachojengwa na
serikali katika eneo la Kizimbani wilaya ya Magharib A mkoa wa Mjini Magharib Unguja.


Amesema serekali imeandaa mazingira wezeshi kwa ajili ya wajasirimali hao kwa kujengea kituo
kitakachowawezesha kufanya shughuli zao kwa kupatiwa mafunzo ya namna ya kuzalisha asali yenye
ubora unaotakiwa, kupatiwa mitaji pamoja na kutafutiwa masoko ya uhakika ya kuuza bidhaa zao.


Amesema vituo hivyo vimewalenga zaidi wajasirimali walio kwenye mfumo wa vikundi ambavyo tayari
vinafanya shughuli hiyo ili kuwawezesha kwa urahisi zaidi ambapo vituo hivyo vitakuwa na vifaa vya
kisasa vitakavyoweza kuchakata asali zaidi ya tani tatu kwa mwaka

Kwa upande wake Katibu Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji anaeshughulikia masuala ya kazi
na Uwezeshaji Khadija Khamis Rajab amesema kituo hicho kitaendeshwa na kusimamiwa na jumuiya ya
wafugaji wa nyuki kuwataka kuvitumia vituo hivyo kwa mujibu wa malengo yaliyokusudiwa kwa mujibu
wa mafunzo waliyopatiwa hapo awali

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Modern Building Contractor Ali Pandu Sharif
amesema wamezingatia ubora uliotakiwa katika ujenzi wa kituo hicho na kuiyomba serikali kuendelea
kuwaamini wakandarasi wazawa na wazalendo katika miradi wanayoweza kuitekeleza ili kuzalisha ajira
nchini

Vituo hivyo vinajingwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika eneo la Kizimbani kwa upande wa
Unguja na eneo la Pujini kwa upande wa Pemba ni kufuatia utekelezaji wa mradi kuwawezesha
wajasiriamali kufuatia Fedha za Ahueni ya Uviko 19 na vinatarajiwa kukamilika tarehe 15 mwezi huu 2022.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »