WAFANYAKAZI SEKTA YA MAWASILIANO WATAKIWA KUIMARISHA UCHUMI SHINDANI WA KIDIGITALI

WAFANYAKAZI SEKTA YA MAWASILIANO WATAKIWA KUIMARISHA UCHUMI SHINDANI WA KIDIGITALI

Na Barnabas Kisengi, Dodoma Katibu mkuu Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Jimmy Yonazi amewataka wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa. Akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao kazi cha uchambuzi

Na Barnabas Kisengi, Dodoma


Katibu mkuu Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Jimmy Yonazi amewataka wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano nchini kukuza maarifa na kuwa na uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa.


Akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa jimmy yonazi amesema kuwa wizara ya mawasiliano imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa na kuwa nchi yenye fursa nyingi ili nchi zingine nazo zije kujifunza hapa nchini.


Aidha Yonazi amesema kila mmoja atambue jukumu lake na siyo kuja ofisini na kurudi nyumbani tu ambapo amewasisitiza kufanya kazi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kimataifa.


“Nawataka kila mmoja ahakikishe anafanya na kutekeleza majukumu yake tusije tu ofidini na kuondoka fanya kazi yako ili kuhakikisha nchi inapiga hatua hata kimataifa”Amesema Jimy Yonazi.


Amesema kuwa serikali imelenga kujenga ufahamu kwa watumishi wa sekta hiyo ya mawasiliano ili kuweza kuwajengea uwezo zaidi katika kuhakikisha wapo vyema na fursa zinakuwa zinajitengeneza ndani na nje ya Tanzania kama wasipofanya hivyo ni wazi watakosa fursa mbalimbali za tehama kimataifa.


”ufahamu kwa watu husika wa kitengo hiki ni muhimu sababu ata mtu anapojitambulisha katokaWizara ya habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari anakuwa anapata ufahari na kujivunia Wizara yake na kupata fursa ndani na nhe ya nchi”Amesema Yonazi
Na kuongeza kuwa “Serikali imeweza kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo watu pamoja na wadau ili kukuza sekta hii ya mawasiliano, kama mnavyo fahamu lazima tutekeleze mipango ya kuangalia yaliyomo ndani ya nchi yetu pamoja na mambo yanayo weza kuhamasisha,”

Aidha ameongeza kuwa inabidi watanzania waangalie nchi wanazotaka kushirikiana nazo ili kuweza kujenga ushirikiano ulio bora katika kukuza wizara ya mawasiliano pamoja na kudumisha suala la ulinzi nakuwapa watu uwanja mpana wakupata ajira.


Kwa upande wake mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Mulembwa munaku amesema kuwa watatekeleza maagizo ya serikali ili kuongza ajira pamoja na pato la Taifa

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »