Mwanasiasa Mkongwe STIVIN WASIRA ateuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa

Mwanasiasa Mkongwe STIVIN WASIRA ateuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa imekutana Jijini dodoma katika kikao halali cha kikatiba kilichoongozwa na Mwenyekiti wa cha cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni RAIS WA JAMUHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA MH SAMIA SULUH HASAN. Akizungumza na waandishi wa habari Katika Ofisi za makao makuu ya chama hicho katibu wa

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Taifa imekutana Jijini dodoma katika kikao halali cha kikatiba kilichoongozwa na Mwenyekiti wa cha cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni RAIS WA JAMUHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA MH SAMIA SULUH HASAN.


Akizungumza na waandishi wa habari Katika Ofisi za makao makuu ya chama hicho katibu wa siasa na uwenezi Komredi Shaka Hamdu Shaka amesema yaliyojiri katika kikao hicho halmashauri kuu CCM Taifa ni uteuzi wa nafasi mbili zilizokuwa wazi za wajumbe wa kamati kuu CCM Taifa ambazo halmashauri kuu imewachagua Mwanasiasa Mkongwe STIVIN WASIRA na Bi TELESIA MTEWE kuwa wajumbe wa kamati kuu CCM Taifa.


Aidha Shaka amesema halmashauri kuu imepongeza chaguzi za mashina na matawi kwa kufanyika vizuri katika kipindi cha uchaguzi uliofanyka hivi karibuni na kuonyesha asilimia 99.9 katika mashina na matawi yote hapa nchini.

Pia halimashauri kuu CCM Taifa imewataka wanancha wa chama cha mapinduzi CCM kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za uchaguzi wa ngazi ya wilayani, Mkoa na Taifa kuanzia Julai 02 mwaka huu ampapo halimashauri kuu CCM Taifa imewataka wananchama kujitokeza ili watumie haki yao ya kikatiba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama cha mapinduzi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »