SAUTI YA WAJANE KUANZIA MASHINANI: WAZIRI DKT. GWAJIMA

SAUTI YA WAJANE KUANZIA MASHINANI: WAZIRI DKT. GWAJIMA

Na Barnabas Kisengi -Dodoma Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inawatambua na kuwaenzi wanawake wote pamoja na makundi maalum wakiwemo wajane. Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inakadiria kuwa idadi ya wajane nchini Tanzania ni laki 8.8 ambayo ni sawa

Na Barnabas Kisengi -Dodoma


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inawatambua na kuwaenzi wanawake wote pamoja na makundi maalum wakiwemo wajane.


Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu inakadiria kuwa idadi ya wajane nchini Tanzania ni laki 8.8 ambayo ni sawa na asilimia 3.1 ya wanawake wote nchini ambao wanakadiriwa kuwa millioni 28.5 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 22,2022 Jijini Dodoma kuelekea siku ya wajane duniani Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima amesema kuwa juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili wajane zinatatuliwa.

“Tunatambua kwamba Maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ni jukwaa linalowaleta pamoja wajane na kuwapa fursa ya kushiriki na kubaini changamoto wanazokumbana nazo na hata kuimarisha ushirikiano kwa ajili ya ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.”Amesema Dkt Gwajima
Gwajima amesema kuongeza kuwa “Tanzania huadhimisha Siku ya Wajane kwa lengo la kukuza hamasa, mshikamano na uelewa ndani ya jamii ili kuacha ukiukaji wa haki za binadamu kwa wajane. Hivyo, kama Taifa, maadhimisho haya yanatoa fursa ya pamoja katika kubaini changamoto za wajane na namna ya kukabiliana nazo katika jamii zetu,”
Ametaja Juhudi ambazo Serikali imekuwa ikizichukua kuwa ni pamoja na Kuitambua Siku ya Wajane Duniani sambamba na kushirikiana na wadau kuweka mikakati ya kutatua changamoto za wajane kama ilivyobainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000, na mpango wa Mkakati wake wa mwaka 2005; Maazimio ya ulingo wa Beijing, Ajenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 na Ajenda ya Maendeleo ya Bara la Afrika 2063Kuelimisha jamii kuacha mila na desturi zenye madhara.

Kuweka na kuimarisha mifumo ya kulinda haki za Wajane kwa kuongezeka kwa huduma za msaada wa sheria kutokana na kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria Na. 1 ya mwaka 2017 ambayo imewezesha makundi maalum ikiwemo wajane na watoto kupata haki zao katika vyombo vya usimamizi wa sheria.
Mwaka 2021 Serikali ilitoa msaada wa kisheria kwa wajane na hivyo kesi 277 za mirathi ziliweza kutolewa hukumu ya ushindi. Hii ni pamoja na uendeshaji wa mashauri na hukumu katika utetezi wa mali.
Kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto 427 katika vituo vya polisi; vituo 153 katika Jeshi la Magereza kwa lengo la kutokomeza ukatili wa Kijinsia kwa Wahanga wakiwemo Wajane.


Kuanzishwa kwa Kampeni ya TWENDE PAMOJA kwa ajili ya kuelimisha jamii kuachana na ukatili wa kijinsia kwa kushirikisha wanaume katika kuelimisha jamii;
Kuhamasisha Wajane kuhamasika kujiunga kwenye vikundi na kuwezeshwa kwenye miradi mbalimbali ya ujasiriamali; Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018, kifungu cha 37A, ambacho kinazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa hizo kutenga asilimia 10 ya Mapato ya ndani (Wanawake 4%, Vijana 4% na Watu wenye Ulemavu 2%) kwa ajili ya kutoa Mikopo na kuleta matokeo makubwa katika kuwezesha wanawake.
Serikali imewezesha kutungwa kwa Sheria ya Ardhi ya Kijiji Namba 5 (1999), Kifungu cha 20(1), ambacho kinatoa nafasi kwa Wanawake kumiliki Ardhi. Hatua hiyo imeleta matokeo ya ongezeko la umiliki wa ardhi kwa wanawake kutoka asilimia 9 (2014) hadi asilimia 25 Mwaka 2017.
Kuwepo kwa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA 2017/18 – 2021/22), ambao unalenga kutokomeza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka huu 2022.


Kwa upande wake Mratibu wa wajane Nchini Mariam Aswile amewataka wajane nchini kutohofia kusimamia rasilimali walizoachiwa na waume zao na kutohofia kuripoti matukio yeyote yanayoashiria ugandamizaji wa haki zao katika jamii na kwa kufanya hivyo itasaidia kuleta haki na usawa katika jamii.
Siku ya Wajane Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 23 Juni mwaka na mwaka huu inabebwa na Kaulimbiu isemayo ” Utu Uwezeshaji wa Kiuchumi na Haki za Kijamii kwa Wajane” ambayo imetokana na Kaulimbiu ya Kimataifa inayosema “Dignity Economic Empowerment and Social Justice for Widows” Kaulimbiu hii inahimiza jamii kuhakikisha kuwa inawathamini wajane kwa kuwapatia haki zao na kuwawezesha kiuchumi na inatukumbusha kuwa, ni jukumu la kila mtu kulinda haki za binadamu na utu wa wajane kwa mujibu wa mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake na ule wa haki za mtoto.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »