MAVUNDE, GAMBO WAZINDUA MCHEZO WA BAO, DODOMA WAIBUKA KIDEDEA

MAVUNDE, GAMBO WAZINDUA MCHEZO WA BAO, DODOMA WAIBUKA KIDEDEA

Na Barnabas Kisengi, Dodoma. Mashindono ya mchezo wa bao ya siku moja ya timu ya Dodoma na Arusha yamezindiliwa na kuchchezwa kwa kuongozwa na Naibu waziri wa kilimo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kuchuana na Mbunge wa Jimbo la Arusha MH MRISHO GAMBO Jijini Dodoma katika viwanja vya

Na Barnabas Kisengi, Dodoma.


Mashindono ya mchezo wa bao ya siku moja ya timu ya Dodoma na Arusha yamezindiliwa na kuchchezwa kwa kuongozwa na Naibu waziri wa kilimo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde kuchuana na Mbunge wa Jimbo la Arusha MH MRISHO GAMBO Jijini Dodoma katika viwanja vya Mambo poa Jijini Dodoma.


Kaitka uzinduzi huu wa mchezo wa bao ulioshirikisha timu mbili Kati ya Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Arusha Dodoma iliwagalagaza Wananchi wa Arusha ambapo Dodoma iliibuka kuwa washindi Katika mchezo huo wa bao.

Awali wakizindua mashindano hayo ya bao mtanange ulikuwa kati ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye Kwa sasa ndiyo Mbunge wa jimbo la Arusha MH MRISHO GAMBO na NAIBU WAZIRI WA KILIMO ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini hadi mtanange wa bao unaisha ngoma ilikuwa groo.
Wakizungumza na wanahabari baada ya mtanange kuisha Mbunge mwenyeji wa Dodoma Mhe. Anthony Mavunde amesema lengo la mchezo huo ni kuweka ujirani mwema kati ya Mkoa wa Arusha na Dodoma na kumwenzi Hayati BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
“Tumeamua kufanya mashindano haya hapa dodoma Jimboni kwangu kwakuwa sasa ile adhima ya Hayati BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE kuwa Dodoma kuwa makao makuu imetimia maana tangu atangaza mwaka 1973 sasa imefikia hatama sasa tunazungumza Dodoma ni makao makuu pia MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE alipo kuwa hapa dodoma alikuwa akienda kucheza mchezo wa bao na Sasa Katika Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewekeza sana katika michezo ndio maana leo tumeamua kucheza mchezo huu ambao ulikuwa umesahulika muda mrefu” amesrma Mavunde.


Aidha Mavunde amesema licha ya Mimi kutoka sare na Mhe. Gambo  bado timu yangu ya Dodoma imeiibuka na ushindi ambao umetufanya kila aingiaye dodoma hata toka katika michezo mbalimbali hapa Jijini.


Kwa upandewake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mhe. Mrisho Gambo amesrma mchezo huo wa bao umekuwa ukisaulikakwa kwa muda mrefu hivyo sasa utakuwa chachu kwa maendeleo hapa nchini.
“Sisi kama wabunge ndio wawakilishi wa Wananchi hapa nchini kwa uzinduzi huu wa leo wa mchuano wa mchezo wa bao hapa Dodoma ambapo licha ya timu yangu kufunga na Mimi kumuonea huruma Mhe. Mavunde kuamua kutoka naye groo Sasa tunataka mchezo huu wa bao tuandae ili Sasa tuanzishe na bungeni tuwe na mashindano ya mchezo wa bao naamini tutakuwa chachu ya kuleta hamasa ya mchezo huu wa bao kwa wabunge na tunapokuwa majimboni kwetu basi tuwe na timu za mchezo wa bao”Amesisitiza Mhe. Gambo

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »