Na Barnabas Kisengi-Dodoma Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma JOSEPH MAFURU amesema ujenzi wa soko la wamachinga wa Jiji la Dodoma umefika asilimia 95 kukamilika na wanategemea ifikapo Julai mosi mwaka huu wafanya biashara hao wahamie na kuanza kufanya biashara zao katika soko hilo. Mategemeo tarehe 1 mwezi 7 mwaka huu ambapo hadi Sasa wafanyabiashara 3000
Na Barnabas Kisengi-Dodoma
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma JOSEPH MAFURU amesema ujenzi wa soko la wamachinga wa Jiji la Dodoma umefika asilimia 95 kukamilika na wanategemea ifikapo Julai mosi mwaka huu wafanya biashara hao wahamie na kuanza kufanya biashara zao katika soko hilo.
Mategemeo tarehe 1 mwezi 7 mwaka huu ambapo hadi Sasa wafanyabiashara 3000 tayari wamejisajiri Kwa mfumo wa kielektroniki kufanya biashara kwenye soko hilo.
MAFURU amesema hayo wakati alipotembelewa na Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT ) wakitembelea soko la wamachinga jijini Dodoma.
Pia MAFURU amemshukuru RAIS SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kuongezae fedha kiasi Cha bilioni 2.5 ili kuweza kuhakikisha wanakamilisha mradi wa soko hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tazania ALAT Mhe. Murshid Ngeze amewaomba viongozi wa mkoa na viongozi wa Majiji kuendelea kutoa Elimu kwa wafanyabiashara wadogo Ili kuwaboreshea na kuwapatia elimu ili kuweza kuwafanya waweze kuafanya biashara zao katika maeneo mazuri na salama na yakiwa rafiki na wateja wao.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *