TANZANIA YAPATA TUZO YA MATANGAZO YA UTALII NCHINI KOREA.

TANZANIA YAPATA TUZO YA MATANGAZO YA UTALII NCHINI KOREA.

Tanzania imefanikiwa kupata Tuzo la kuwa na banda bora lenye ubunifu wakutangaza utalii katika maonesho ya 37 ya utalii ya Seoul International Travel Fair(SITF). Maonesho hayo yaliyofanyika katika jiji la Seoul nchini Korea Kusini kuanziatarehe 23 – 26 Juni 2022.“Tuzo hii ni ishara nzuri ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini KoreaKusini, Bodi ya

Tuzo ya Banda Bora la Tanzania lenye ubunifu wa matangazo ya utalii.
Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Edriss Mavura akipokeaTuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Maandalizi ya maonesho ya SITF, Mhe. Shin, Joong-
mok.

Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Balozi Togolani Edriss Mavuraakimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Maandalizi ya Maonesho ya SITF, Mhe. Shin,
Joong-mok.


Tanzania imefanikiwa kupata Tuzo la kuwa na banda bora lenye ubunifu wa
kutangaza utalii katika maonesho ya 37 ya utalii ya Seoul International Travel Fair
(SITF). Maonesho hayo yaliyofanyika katika jiji la Seoul nchini Korea Kusini kuanzia
tarehe 23 – 26 Juni 2022.
“Tuzo hii ni ishara nzuri ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini Korea
Kusini, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na wadau wa Utalii wa Tanzania katika
kuandaa ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya SITF. Tutaendelea kuzijongea
fursa za kutangaza utalii wa Tanzania na kushiriki katika matukio mbalimbali
yatayofanyika hapa Korea”.
Hayo ameyasema Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Edriss
Mavura wakati anakabidhiwa Tuzo hiyo na Mwenyekiti wa Maandalizi ya maonesho
ya SITF, Mhe. Shin, Joong-mok. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Banda la
Tanzania.
Banda la Tanzania lilipambwa kwa kuonyesha vivitio mbalimbali vinavyopatikana
nchini Tanzania ambapo picha za Utalii wa kutamaduni, Mlima Kilimanjaro, fukwe
za Zanzibar, nyumbu wanaovuka Mto Mara, na madini ya Tanzanite zimewavutia
wageni wengi waliotembelea maonesho hayo.
Katika Banda la Tanzania wananchi wa Korea waliweza kujitokeza kwa wingi
kunywa na kufurahia radha ya kahawa ya Tanzania , Tukio hili lilichangia Banda la
Tanzania kutembelewa na wageni wengi.. Kahawa iliyotumika kwenye maonesho
haya ni ile inayolimwa katika wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma.
Aidha, Wanawake wengi wa waliotembelea banda la Tanzania walivutiwa sana na
usisi wa nywele ambapo walijitokeza kwa wingi kusuka nywele zao. Jambo ambalo
walionyesha kulifurahia sana.
Kwa upande wa Bodi ya Utalii Tanzania, Afisa Habari na Uhusiano, Bi, Augustina
Makoye amesema “Tunaendelea kubuni njia mbalimbali za kutangaza utalii wa
Tanzania ili vivutio vya Tanzania viweze kujulikana zaidi katika soko hili ambalo
wananchi wengi wameonyesha kuvutiwa zaidi na vitu vya kiutamaduni, tutaendelea
kuliwekea mkakati wa kutangaza utalii wa kiutamaduni kwa vitendo ili tuweze
kuwavitia watalii wengi wa nchi ya Korea Kusini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »