SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA WA MAKOMBE| HII HAPA CV YAKE

SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA WA MAKOMBE| HII HAPA CV YAKE

Klabu ya Simba SC, leo Jumanne, Juni 28, 2022 imemtangaza Zoran Manojlovic (Zoran Maki) kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Pablo Franco Martini. –Simba imempa kazi kocha huyo baada ya kujiridhisha ambapo Zoran amewahi kuzifundisha klabu mbalimbali kama vile Primeira De Agosto,Wyadad AC,Al Hilal,CR Belouizdad na Al Tai. –Maki raia wa

Klabu ya Simba SC, leo Jumanne, Juni 28, 2022 imemtangaza Zoran Manojlovic (Zoran Maki) kuwa Kocha Mkuu mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Pablo Franco Martini.

–Simba imempa kazi kocha huyo baada ya kujiridhisha ambapo Zoran amewahi kuzifundisha klabu mbalimbali kama vile Primeira De Agosto,Wyadad AC,Al Hilal,CR Belouizdad na Al Tai.

–Maki raia wa Ureno aliwahi kufutwa kazi na Al Hilal Club mwaka 2021 baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi mbili za kwanza za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambapo alipata sare dhidi ya TP Mazembe na kufungwa dhidi ya Mamelodi.

–Pia Utakumbuka mwaka 2020, Zoran alifutwa kazi katika klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco baada ya kutoka sare ya 2-2 na klabu ya Petro Atletico ya Angola katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika ikiwa ni miezi 6 tu tangu atangazwe kuwa kocha wa klabu hiyo.

–Mafanikio yake makubwa ni kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2018 akiwa na klabu ya Primeiro De Agosto.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »