WIZARA YA AFYA KUSHIKIRIANA NA ‘MAMA ONGEA NA MWANAO’ KUBORESHA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

WIZARA YA AFYA KUSHIKIRIANA NA ‘MAMA ONGEA NA MWANAO’ KUBORESHA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Na Mwandishi WETU Dodoma Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel  amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao akiwemo Steven Nyerere pamoja na Vyonne Cherrie (Monalisa) katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu malengo ya taasisi hiyo kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto

Na Mwandishi WETU Dodoma


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel  amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao akiwemo Steven Nyerere pamoja na Vyonne Cherrie (Monalisa) katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.


Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu malengo ya taasisi hiyo kuhakikisha kwamba afya ya mama na mtoto inaboreshwa hasa katika kipindi kigumu cha mama kujifungua.


Viongozi hao wamesema taasisi hiyo imeamua kujikita katika eneo la afya ya mama na mtoto baada ya kufanya utafiti mdogo katika mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na ukanda wa kati na kujiridhisha kuwa eneo hilo linahitaji ufumbuzi na usimamizi wa karibu.
 Viongozi hao wamesema taasisi hiyo kupitia washirika wameanzisha kampeni iitwayo “Jali afya ya mama na mtoto” ambapo itasaidia maboresho katika maeneo muhimu ikiwemo ujenzi wa zahanati, ununuzi wa vifaa tiba kama vile Ultra Sound pamoja na vifaa vyote vinavyohusu afya ya na mtoto.


Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Mollel ameishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya nchini hasa afya ya mama na mtoto na amesema Wizara ya Afya iko tayari kutoa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza malengo ya taasisi hiyo ikiwemo kutoa taarifa kamili ya maeneo yenye upungufu wa huduma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »