WAZIRI SIMBACHAWENE ASEME SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA SEKTA BINAFSI KUDHIBITI UKIMWI

WAZIRI SIMBACHAWENE ASEME SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA SEKTA BINAFSI KUDHIBITI UKIMWI

NA Barnabas Kisengi ,DODOMA Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kuhakikisha inafikia azma ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU)kwa asilimia 100  kwa vijana ili kuwapa nafasi ya kutimiza malengo yao. Simbachawene amesema hayo wakati wa

NA Barnabas Kisengi ,DODOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kuhakikisha inafikia azma ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU)kwa asilimia 100  kwa vijana ili kuwapa nafasi ya kutimiza malengo yao.


Simbachawene amesema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji na usambazaji wa vishikwambi kwa ajili ya kufundishia elimu ya VVU na ugonjwa wa  Ukimwi, afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa timiza malengo kwa wasichana balehe na Wanawake vijana.


Waziri Simbachawene amesema, maendeleo ya nchi yanategemea nguvu kazi ya rasilimali watu na nguvu kazi hiyo kwa sehemu kubwa inafanya na vijana hivyo utekelezaji wa mradi wa timiza malengo kwa wasichana balehe na Wanawake vijana utasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru kundi hilo kwenye maambukizi ya VVU.
“Pamoja na  jitihada zinazofanywa na serikali kulinda kundi hili yapo masuala kadhaa ikiwemo maambukizi ya VVU na UKIMWI  ambayo yamekuwa ni kikwazo kikubwa Kwa ustawi wa Vijana na Taifa kwa ujumla,ugonjwa wa  UKIMWI umeendelea kuwa tishio la uchumi na maendeleo ya nchi na madhara yake yanaendelea kuwa ni changamoto katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa,”amesema Simbachawene.


Hata hivyo Simbachawane alisisitiza kuwa kama Taifa kuna kila sababu ya kuhakikisha kundi la vijana linalindwa ili kuimarisha nguvu kazi ya Taifa,kukuza uchumi,na kujenga Taifa lenye nguvu na kuongeza kuwa yapo mengi ambayo serikali inafanya kuhakikisha kundi hilo linawekewa mazingira wezeshi na salama yanayolinda ustawi wa akili  na miili yao.


Amesema kuwa njia muhimu zitakazoweza kudhibiti maambukizi ya VVU Kwa vijana ni Kwa njia ya elimu  kuhusu masuala ya UKIMWI ili kusaidia kundi hilo kutimiza malengo.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaridhishwa sana na namna mradi wa timiza malengo unavyotekelezwa kwa maslahi mapana ya Taifa mradi huu ulianza katika mikoa mitatu na halmashauri 10 wamepanua wigo hadi kufikia mikoa mitano na halmashauri 18,”amesema Simbachawene.


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania  (TACAIDS) Dk. Leonard Maboko alisema mradi wa timiza malengo  unagharimu fedha sh.bilion 55.2  na unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria (Global Fund) katika mikoa mitano.


Amesema mradi huo unatarajia kuwafikia wasichana belehe na wanawake vijana walioko nje na ndani ya mfumo wa shule wapatao million 1 lengo ikiwa ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu maambukizi ya UKIMWI ili kukuza nguvu kazi ya Taifa.
“Msingi wa utekelezaji wa mradi huu ni kusaidia kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 ili waweze kutimiza Malengo  Malengo na ndoto zao pasipo kikwazo chochote
Amesema kuwa mradi huo unalenga kusaidia wasichana walio ndani na nje ya mfumo wa shule kwa kuwajengea uwezo kifikra ,maarifa na maadili ili wakati wote wabaki salama dhidi ya maambukizi ya VVU  na waweze kutumika na kulijenga Taifa.


Kwa upandewake Lilian Sadala Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Mtumba aliishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali vijana kwani wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali ambazo zimepelekea wengine kukatisha ndoto zao.
Amesema elimu ya ukimwi ni muhimu kwa vijana kwasababu itasaidia Kwa wanafunzi ambao wapo katika umri wa kubalehe ambao mara  nyingi huaribikiwa  Kwa kujiunga na makundi yasiyoeleweka

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »