UDOM KUJENGA MATAWI 20 AFRIKA

UDOM KUJENGA MATAWI 20 AFRIKA

CHUO Kikuu cha  Dodoma (UDOM) kimedhamiria kuwa kati ya  Vyuo Vikuu 20 bora Barani Afrika ifikapo Mwaka 2030 kwa kuzalisha Waatalamu mahiri na wenye uwezo mkubwa wanaoendana na soko la ajira. Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Faustine Bee ameyasema hayo hii Leo  Jijini Dodoma katika kilele cha maonesho ya bunifu mbalimbali za wanafunzi wa Ndaki

CHUO Kikuu cha  Dodoma (UDOM) kimedhamiria kuwa kati ya  Vyuo Vikuu 20 bora Barani Afrika ifikapo Mwaka 2030 kwa kuzalisha Waatalamu mahiri na wenye uwezo mkubwa wanaoendana na soko la ajira.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Faustine Bee ameyasema hayo hii Leo  Jijini Dodoma katika kilele cha maonesho ya bunifu mbalimbali za wanafunzi wa Ndaki ya Sanyansi Asilia na Hisabati  yaliyofanyika katika Chuo Kikuu hicho.

Aidha Profesa Bee amesema kuwa kama Chuo wataendelea kuboresha Mitaala ya sayansi katika kuleta mabadiliko ya kushughulikia changamoto za kibinaadamu.

Rasi wa Ndaki ya Sayansi asilia na Hisabati Profesa Said Ally Vuai amesema mpaka sasa wamepiga hatua katika tafiti mbalimbali na wanao wataalam wakutosha.

Awali baadhi ya Wanachuo wa Sayansi asilia na Hisabati wakaonyesha bunifu mbalimbali walizozifanya kutokana na uwezo walio nao.

Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)  malengo yake ni kuzalisha Waataalamu watakaolisaidia Taifa katika utekelezaji wa shughuli zake pamoja na jamii. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »