MAJALIWA: RAIS SAMIA AMETOA SH. BILIONI MBILI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO NANGANGA

MAJALIWA: RAIS SAMIA AMETOA SH. BILIONI MBILI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO NANGANGA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Nanganga wilayani Ruangwa. Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 4, 2022) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata hiyo akiwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata ya Nanganga wilayani Ruangwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 4, 2022) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo ya afya, elimu na maji.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa umwagiliji Nanganga, tutumie vizuri bonde letu. Vijana changamkieni fursa hii kwa kuanzisha kilimo cha mbogamboga na mazao mengine.”

 Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa uendelee na mpango wa ujenzi wa soko la mboga mboga katika Kata ya Nanganga ili kuwawezesha wakulima wa mazao hayo kupata sehemu ya uhakika ya kufanyia biashara.

Amesema Serikali imetoa shilingi milioni 447 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji maji Nanganga na shilingi milioni 31 kwa ajili ya kusambaza maji katika kijiji cha Mbecha na shilingi milioni 470 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Mchenganyumba.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi wajitahidi kusoma kwa bidii kwa sababu mbali na Serikali kutoa Elimsingi Bila Ada pia imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya kutolea elimu nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Nangumbu, zahanati ya kijiji cha Mtakuja pia, ametembelea shule ya msingi Ndandawale pamoja na kuwasamia wananchi wa kijiji cha Chimbila na kuwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa bidii Serikali ipo pamoja nao.

Awali, Diwani wa Kata ya Nanganga, Bw. Kambona aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo miradi ya maji ambayo imeweza kutatua changamoto ya uapatikanaji maji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »