BAHI: WAZIRI BITEKO AWAPA SIKU SABA WACHIMBAJI WA MADINI KULIPA DENI LA WANANCHI

Na Mwandishi Wetu Bahi Dodoma Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko, ametoa siku Saba kwa wachimbaji wa madini ya Chuma wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma kulipa madeni wanayodaiwa na wananchi katika migodi hiyo kwa wanaofanya kazi ya kuponda madini hayo. Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Asanje mara baada ya kutembelea

Na Mwandishi Wetu Bahi Dodoma


Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko, ametoa siku Saba kwa wachimbaji wa madini ya Chuma wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma kulipa madeni wanayodaiwa na wananchi katika migodi hiyo kwa wanaofanya kazi ya kuponda madini hayo.


Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Asanje mara baada ya kutembelea maeneo ya wachimbaji wa chuma na kupokea malalamiko.


Dkt.Biteko, amemwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kusimamia agizo hilo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ili wanachi hao wa Asanje walipwe fedha zao wanazowadai wawekezaji hao.
“Mkuu wa wilaya, kama kuna mtu atakuwa hajalipwa hadi jumatatu Afisa Madini unasimamisha mgodi huo mara moja bila masharti yoyote, uandike kabisa kwa maelekekeao ya Waziri nasimamisha,” amesisitiza Dkt Biteko.


Aidha Waziri Dkt Biteko amewataka wachimbaji wa madini na wawekezaji katika Sekta ya Madini kuhakikisha wanashirikisha wananchi katika mipango yao ya uwekezaji kabla hawajawekeza kwenye miradi hiyo ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.

Amesema, ushirishwaji utasaidia kujua vipaumbele vya wanachi ili iwe rahisi kwa utekelezaji.
“Nataka niwaambieni  leseni hizi mmepewa kwa niaba ya Watanzania wengine. Kwa kuwa tumewapa wenzetu leseni ya kuchimba matarajio ya Serikali ni kwamba hawawezi kugeuka tena kuwa kero kwa watu ambao wako maeneo ya kuchimba,”amesema Dkt Biteko.


Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nollo amesema, ziara ya Dkt.Biteko katika Kijiji cha Asanje kusikiliza malalamiko ya wanachi hao, imekuwa na manufaa kwa wananchi na matarajio makubwa katika shughuli za uchimbaji madini.


Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda amemshukuru Dkt.Biteko kwa kuweza kufika na kusikiliza changamoto za wananchi hao kwani ilikuwa ni kiu kubwa ya kuweza kufikisha malalamiko yao kwake.Wilaya ya Bahi yanapatikana madini mbalimbali yakiwemo dhahabu, chuma na madini ujenzi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »