“WAZIRI UMMY UMELITENDEA HAKI TAIFA UNASTAHIKI PONGEZI” MHE. HEMED MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR.

“WAZIRI UMMY UMELITENDEA HAKI TAIFA UNASTAHIKI PONGEZI” MHE. HEMED MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman amesema katika suala zima la kuendelea kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchini ipo haja kwa Wataalamu wa Sekta za Mazingira Nchini kuangalia kwa kina uvamizi wa Maji ya Bahari yanayoendelea kukiathiri Kijiji cha Sipwese kiliopo Mkoa Kusini Pemba. Mheshimiwa Hemed Suleiman amesema hayo wakati

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Ali Mwalimu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Ummy Ali Mwalimu akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman amesema katika suala zima la kuendelea kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchini ipo haja kwa Wataalamu wa Sekta za Mazingira Nchini kuangalia kwa kina uvamizi wa Maji ya Bahari yanayoendelea kukiathiri Kijiji cha Sipwese kiliopo Mkoa Kusini Pemba.

Mheshimiwa Hemed Suleiman amesema hayo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia masuala ya Muungano na Mazingira wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ummy Ali Mwalimu aliyefika kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amempongeza Waziri Ummy Ali Mwalimu kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo ambayo pamoja na mambo mengine inahusika moja kwa moja na masuala ya Muungano ambae ana sifa zote hasa kutokana na umakini wake wa kuitendea Haki Tanzania wakati wa Taifa lilipopata maambukizi ya Virusi vya Corona wakati akiwa Waziri aliyesimamia masuala ya Afya.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mheshimiwa Ummy Ali Mwalimu amesema Wizara yake imepewa kazi nzito ya kuratibu masuala ya Muungano sambamba na Mazingira kwa pande zote mbili.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia Muungano na Mzingira Mhe. Ummry Ali Mwalimu alikutana kwa mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Sera, Uratibu na Shughuli za Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohamed.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Vuga Mjini Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed amesema pande hizo mbili zinapaswa kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika Taasisi za Kiutendaji badala ya kusubiri kutatua Kero za Muungano.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Disemba 23, 2020.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »