RAIS DKT. MWINYI ATOA MKONO WA POLE

RAIS DKT. MWINYI ATOA MKONO WA POLE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo amefika Nyumbani kwa Mfanyakazi wake kutoa mkono wa pole baada ya kifo cha Baba Mzazi wa Mfanyakazi huyo huko nyumbani kwao Dole,Ndunduke Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) leo amefika Nyumbani kwa Mfanyakazi wake kutoa mkono wa pole baada ya kifo cha Baba Mzazi wa Mfanyakazi huyo huko nyumbani kwao Dole,Ndunduke Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisalimiana na wanafamilia wa Marehemu Bw.Mohamed Ali Juma mume wa Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma alipofika  Nyumbani kwao Bububu Kijichi Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi kutoa mkono wa pole.[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati)  alipofika  Nyumbani kwa  Mbunge wa Jimbo la Bububu Mhe.Mwantakaje Haji Juma (wa pili kulia) leo  kutoa Mkono wa pole baada ya kufiliwa na mume wake Marehemu  Mohamed Ali Juma,  Kijichi Wilaya ya Magharibi”A” Mkoa wa Mjini Magharibi .[Picha na Ikulu] 08/Julai 2022. 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   Mapinduzi  Alhaj Dk. Hussein Mwinyi amejumuika na waumin mbali mbali katika Ibada ya  Sala ya  Ijumaa iliofanyika Msikiti wa Ijumaa Miembeni, Mkoa Mjini Magharibi.

Mapema, akisoma hotuba ya Sala hiyo ya Ijumaa, Khatibu wa Msikiti huo Sheikh Khalid Ali Mfaume, aliwataka waumini kutumia vyema siku kumi za mwanzo wa Mwezi huu wa Mfunguo tatu (Dhulhijjah) kwa kudumisha ibada kwa ajili ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu.

Akielezea miongoni mwa Ibada hizo, Sheikh Khalid ambae pia ni katibu Mtendaji ofisi ya Mufti wa Zanzibar alizitaja kuwa ni pamoja na kuchinja kuambatana na sifa na aina za wanyama wanaofaa kuchinjwa, wakati wa kuchinja na namna ya ugawaji wa kile kilichochinjwa.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa waumini kuendeleza malezi bora yatakayowafanya wazazi kuwa na ukaribu na watoto wao, hali inayojenga urafiki na akatolea mfano wa kisa cha Nabii Ibrahim (AS) na mwanawe Nabii Ismail (AS).

Wakati huo huo, Alhaj Dk. Mwnyi alipata fursa ya kufika nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Bububu (CCM) Bi Mwantakaje Haji Juma kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kufiwa na  mumewe pamoja na kufika Dole Ndunduke kutoa mkono wa pole kwa Mfanyakazi wa Ofisi yake kutokana kifo cha Baba yake mzazi Marehemu Hamdoun Suleiman Soraga.        

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »