RAIS DK.MWINYI KATIKA DUA YA KITAIFA PAMOJA NA CHAKULA NA MAYATIMA

RAIS DK.MWINYI KATIKA DUA YA KITAIFA PAMOJA NA CHAKULA NA MAYATIMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza haja kwa jamii kujitahidi kuwajengea mazingira mazuri yatima yatakayowapa fursa na kuwaondolea huzuni na ukiwa wa kuondokewa na wazazi wao. Alhaj Dk. Mwinyi ameeleza hayo leo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake katika dua ya Kitaifa pamoja na dhifa ya chakula

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza haja kwa jamii kujitahidi kuwajengea mazingira mazuri yatima yatakayowapa fursa na kuwaondolea huzuni na ukiwa wa kuondokewa na wazazi wao.

Alhaj Dk. Mwinyi ameeleza hayo leo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake katika dua ya Kitaifa pamoja na dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya watoto yatima, hafla iluyoandaliwa na Jumuiya ya Nuru Foundation kwa kushirikiana na Jumuiya mbali mbali pamoja na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, iliyofanyika katika uwanja vya Mao Tse Dong, Zanzibar.

Katika hotuba yake hiyo, Alhaj Dk. Mwinyi aliwahimkiza walimu katika taasisi zote za elimu ya dini na sekula kuhakikisha kwamba wanaweka mazingira maalum kwa watoto yatima katika utoaji wa huduma, malezi, misaada na fursa mbali mbali zinazotolewa katika jamii.

Alhaj Dk. Mwinyi alihimiza juu ya umhimu wa wazazi kushirikiana na kuongeza bidii katika malezi ya watoto na kuitaka jamii kutekeleza wajibu wake huo kwani bila ya shaka wakiwalea watoto vizuri, itakuwa rahisi kufahamu umuhimu wa kuishi na wenzao walio yatima.

“jambo hili litawezekana iwapo tutajenga mahusiano mema tokea wakiwa nyumbani, skuli, kwenye madrasa na katika mikusanyiko yote ndani ya jamii….Tujue kuwa sote ni wazazi na walezi kwao”, alisema Alhaj Dk. Mwinyi.

Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa Jumuiya ya Nuru Foundation kwa juhudi inazoendelea kuzichukua katika kuimarisha malezi na ustawi wa watoto yatima katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Mwinyi alieleza kwamba suala la kuiombea dua nchi ni wajibu kwa kila mwananchi na kusisitiza haja ya kuendelea kuhimizana na kukumbushana kila pale inapopatikana nafasi.

Hivyo, Alhaj Rais Dk. Mwinyi amekubali ombi la Serikali kuwekwa siku maalum kwa ajili ya tukio kama hilo kila mwaka kwa azma ya kuwafariji yatima, kula nao pamoja na kuiombea dua nchi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Kwa upande wa Zanzibar Alhaj Dk. Mwinyi alieleza kwamba nguvu za kiuchumi bado ni ndogo lakini Zanzibar bado inaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa kuishi katika hali ya amani na utulivu.

“Sote tunaamini kwamba matumizi bora ya rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu ameibariki Zanzibar kwanza yanategemea kuwepo kwa hali ya amani, utulivu, umoja na mshikamano uliopo katika maisha ya kila siku.

Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa viongozi wa dini mbali mbali kwa kuendelea kuiombea dua nchi pamoja na kuhubiri amani na utulivu huku akiupongeza uamuzi wa kuifanya shughuli hiyo ya dua kwa kuandaa dhifa ya kitaifa ya watoto yatima katika kipindi hichi cha sikukuu.

Aliongeza kwamba katika utamaduni wa Zanzibar tangu hapo zamani wazee hata wale waliokuwa na uwezo mdogo wa kiuchumi walijitahidi kufanya maandalizi ya sikukuu kwani siku ya sikukuu huwa ni maalum lakini kubwa ni siku ya furaha na zaidi kwa watoto.

Alisisitiza haja ya kusaidiana na kushirikiana katika kuwatunza yatima na kukubali rai ya uratibu wao ili iwe rahisi kuwasaidia na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Katika hafla hiyo, Alhaj Dk. Mwinyi pamoja na Mama Mariam Mwinyi walitoa mchango wa TZS Milioni kumi (10,000,000) kati ya milioni hamsini (50,000,000) zilizohitajika na kuongoza harambee iliyopelekea kupatikana zaidi ya kiwango hicho cha fedha kilichoombwa.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya shughuli hiyo Mama Zainab Othman Masoud, Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alieleza mambo yaliyomgusa na kuamua kufanya tukio hilo huku akitoa shukurani kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa taasisi na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika kufanikisha shughuli hiyo.

Viongozi wa dini nao kwa upande wao walieleza umuhimu wa kuwatunza mayatina sambamba na kueleza athari za kula mali za yatima huku wakisisitiza haja ya kuwasaidia mayatima hasa ikizingatiwa kwamba dini si kusali peke yake bali kuna mambo mengi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu ikiwemo kuwatunza yatima.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »