“TEHAMA ITUMIKE KATIKA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI” MH.MAJALIWA

“TEHAMA ITUMIKE KATIKA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI” MH.MAJALIWA

23 Desemba, 2020  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TEHAMA ITUMIKE KATIKA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali ili kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini

23 Desemba, 2020 

washiriki

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TEHAMA ITUMIKE KATIKA KUONGEZA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali ili kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini pamoja na kuongeza ajira.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Desemba 23, 2020) katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi mashindano ya TEHAMA yaliyoandaliwa na kampuni ya HUAWEI ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili kidunia na ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahala na Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapongeza washindi na waandaaji wa mashindano hayo. Hafla hiyo imefanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kufikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye maeneo mengi zaidi kwa lengo la kuongeza matumizi ya mawasiliano ya kasi (broadband) kutoka asilimia 45 ya sasa hadi asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu amesema ili kufikia malengo hayo, Serikali itatoa kipaumbele kwenye masuala ya tafiti na ubunifu sanjari na kutambua na kusajili wataalamu wote wa TEHAMA nchini. 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUUJUMATANO, DESEMBA 23, 2020.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »