ASIMILIA 37 YA WATANZANIA WAMEPATA CHANJO YA UVIKO-19

ASIMILIA 37 YA WATANZANIA WAMEPATA CHANJO YA UVIKO-19

Na.Catherine Sungura,Tanga Hadi kufikia tarehe  Julai 18 2022 jumla ya wananchi milioni 11.5 sawa na asilimia 37 ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamepata chanjo kamili ya UVIKO-19 hapa nchini. Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni

Na.Catherine Sungura,Tanga


Hadi kufikia tarehe  Julai 18 2022 jumla ya wananchi milioni 11.5 sawa na asilimia 37 ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamepata chanjo kamili ya UVIKO-19 hapa nchini.


Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni mkakati wa uhamasishaji wa kuongeza kasi ya kuchanja nchini.
“Tumeshachanja watu milioni 11.5 wamepata kinga kamili kati ya watu milioni 30.7 ambao tumewalenga, sasa hivi imethibitika pasi na shaka kwamba chanjo ndio njia pekee ya uhakika inayoweza kupunguza makali ya UVIKO-19 na ili tuweze kutengeneza kinga ya jamii, dunia imejiwekea malengo angalau tuweze kuchanja asilimia 70 ya watu wote duniani” Amesema Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy amebainisha kwamba   idadi hiyo imefikiwa kutokana na kampeni iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan mwaka 2021 ikiwemo huduma tembezi, kusogeza vituo vya kuchanja karibu na  maeneo ya watu ambapo vituo vya kutolea chanjo vilikua  550 mwaka 2021 na kufikia vituo 7000 mwaka 2022.


Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na itaendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi za dini hapa nchini katika mapambano dhidi ya magonjwa ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 hivyo kikao hicho kitaleta mbinu mbalimbali za kuwafikishia wananchi.
“Tunaamani kabisa ninyi viongozi wa dini mnajihusisha kwenye mambo ya jamii mna mambo makubwa ya kutufundisha na mtatupatia mbinu na mikakati mbalimbali za kwenda kuwahamasisha wananchi, ninyi tangu ugonjwa huu kuingia nchini mmekua mnatusaidia  kufikisha elimu kwa jamii kujikinga na ugonjwa huu” amesema Waziri Ummy
Kuhusu hali ya uchanjaji kwa Mkoa wa Tanga Waziri Ummy amesema Mkoa wa Tanga ipo asilimia 22 kati ya asilimia 37 ya Kitaifa na  Wilaya ya Muheza  wamechanja asilimia 69 na kufuatiwa na Pangani asilimia 40, Korogwe mji 38, handeni mji 35 na Tanga jiji asilimia 26.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »