Na Mwandishi Wetu, Watu 10 wakiwemo wanafunzi 8, dereva na mwanamke mmoja wamefariki dunia na wengine 18 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la shule ya king David iliyotokea mapema leo asubuhi Mjini Mtwara wakati wakielekea shuleni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo “Nimepokea salamu za rambirambi kutoka

Na Mwandishi Wetu,
Watu 10 wakiwemo wanafunzi 8, dereva na mwanamke mmoja wamefariki dunia na wengine 18 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la shule ya king David iliyotokea mapema leo asubuhi Mjini Mtwara wakati wakielekea shuleni

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
“Nimepokea salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ametutakia pole wakazi wa Mtwara katika kipindi hiki kigumu… niwaombe madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani” alisema Gaguti
Ajali hiyo iliyohusisha basi namba T207 CTS aina ya town hiace ilipata ajali katika mteremko wa Mjimwema baada ya kufeli kwa breki na kupoteza mwelekeo majira ya saa moja asubuhi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo amesema uchunguzi wa awali unaonesha breki za gari hilo zilifeli na kusababisha kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye gema
“Majeruhi 18 wanaendelea kupatiwa matibabu kati yao Watano wapo katika chumba uangalizi maalum” alisema Katembo
Aliongeza kuwa “dereva wa gari hilo, mama mmoja aliyeomba lifti na wanafunzi 8 wamefariki dunia”

Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *