Na Barnabas Kisengi, Dodoma Serikali imetoa kauli juu ya kuibuka kwa ugonjwa wa Homa ya mgunda uliotokea huko mkoani Lindi na kuenea kwa taarifa zinazodai kuwa nyama si salama kukiwa.Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa huduma za mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga wakati akizungumza na waandishi wa Habari
Na Barnabas Kisengi, Dodoma
Serikali imetoa kauli juu ya kuibuka kwa ugonjwa wa Homa ya mgunda uliotokea huko mkoani Lindi na kuenea kwa taarifa zinazodai kuwa nyama si salama kukiwa.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa huduma za mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutolea ufafanuzi suala hilo ambapo amesema nyama inayouzwa kwenye mabucha yaliyosajiliwa ni salama na haina vimelea vya ugonjwa huo.
Aidha Prof. Nonga amewatahadharisha wananchi wenye tabia ya kula nyama za wanyama kama panya na popo kwani ni wanyama wenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuepuka mwingiliano na wanyamapori.
Kwa upande wake msajili wa bodi ya nyama Tanzania Dkt. Daniel Mushi amesema Bodi hiyo inafanya kazi ya ukaguzi kwenye mabucha yote hapa nchini ili kuhakikisha nyama inayouzwa inakuwa salama Kwa matumizi ya binadamu.
“Tumekuwa tukifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maduka ya kuuzia nyama na kukagua ili kuhakikisha nyama inapo mfikia mlaji ikiwa salama kwa matumizi ya binadamu” amesema Dkt Mushi.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *