WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA VIJANA KUTAMBULIWA KWENYE MIKOPO YA 10%

WAZIRI NDALICHAKO AAGIZA VIJANA KUTAMBULIWA KWENYE MIKOPO YA 10%

Ña Angela Msimbira OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watuwenye  Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako  ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi  ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.Amesema hayo Julai 27,2022 Jijini Dodoma

Ña Angela Msimbira OR-TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watuwenye  Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako  ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi  ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.
Amesema hayo Julai 27,2022 Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa  wakati akifunga rasmi  program ya Feed  the Future  Tanzania inua vijana chini Tanzania chini ya ufadhili wa  Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani,USAID Tanzania.


Prof Ndakichako amesema kuwa vijana ni nguzo na rasilimali muhimu katika Taifa hivyo Serikali imekuwa ikuchukua hatua  za kuhakikisha kwamba inaleta ustawi kwa vijana  na kuweka  Mazingira wezeshi ya kuweza  kupata maendeleo, hivyo kila Halmashauri inawajibu wa kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kichumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.
Prof. Ndalichako ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kushirikiana na  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuhakikisha Vijana wanaedelea kuwezeshwa kwa kujengewe uwezo na kupewa vitendea kazi ili waweze kujikwamu kiuchumi Na kuleta maendeleo nchini.


Aidha, Prof. Ndalichako amezitaka Wizara na Taasisi zote zinazohusiana na ustawi wa jamii kushirikiana kwa pamoja kwa kuweka Mpango Mkakati wa kushughulika changamoto zinazoakabili vijana wa makundi yote nchini. 
Akiongea kwa Niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkurugenzi  wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI  Victor Kategere amelishukuru shirika  la Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani,USAID Tanzania kwa kuwainua vijana kiuchumi na kuwapongeza Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zilizonufaika na mradi huo kwa usimamizi uliotukuka.


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, Kate Somvongisiri amesema Programu hiyo imehusisha vijana wa vijijini wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kujihusisha na biashara ya kilimo na minyororo mingine ya thamani na kuongeza fursa zao za kiuchumi huku wakikuza uongozi na maisha bora.
” Tunajivunia kuwa mradi huu Inua Vijana umewafikia zaidi ya vijana 43,000 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3 (dola za Marekani milioni 2.3) kama ruzuku kwa biashara na kilimo zinazomilikiwa na vijana.”amesema Somvongisiri.


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amesema kwa Mkoa wa Mbeya, vijana 14,000 wamenufaika na kati ya hao vijana 1,000 wamefikia mafunzo ya uongozi, vijana 3,000 wamepata mafunzo ya ujasiliamali na takribani vijana 10,000 wamefikia na mafunzo ya stadi za maisha.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amewataka vijana walionufaika na programu ya Feed the Future kutumia mafunzo hayo kuzalisha na kupiga hatua na kuleta faida kwa jamii inayowazunguka.


Aidha, Programu ya The Feed the Future imetumia zaidi ya Tsh.Bilioni 8 katika kuwezesha vijana, Mikoa iliyonufaika na Mradi huo ni Iringa na Mbeya kwa upande wa Tanzania Bara, unguja na Pemba kwa Tanzania Visiwani.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »