SERIKALI KUONGEZA VITUO VYA AFYA YA AKILI NCHINI

SERIKALI KUONGEZA VITUO VYA AFYA YA AKILI NCHINI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma SERIKALI imesema itaendela kuongeza vituo vya huduma ya afya ya akili nchini ili kuboresha utoaji wa huduma hiyo kwa lengo la kukabiliana na afya ya akili.Mratibu wa Hospitali za afya ya akili Tanzania Oresmos Mndeme amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua huduma ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu afya ya akili.

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


SERIKALI imesema itaendela kuongeza vituo vya huduma ya afya ya akili nchini ili kuboresha utoaji wa huduma hiyo kwa lengo la kukabiliana na afya ya akili.
Mratibu wa Hospitali za afya ya akili Tanzania Oresmos Mndeme amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua huduma ya utoaji elimu kwa jamii kuhusu afya ya akili.


Aidha Mratibu huyo amesema kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya Wgonjwa wa afya ya akili takribani milioni sita hadi saba hivyo wataendelea kubuni program mbalimbali za utoaji elimu kwa lengo la kuifikia jamii ya Tanzania kukabidiana na ugonjwa huo wa afya ya akili.


Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe Dr Paulo Lawala ameeleza lengo la uzinduzi wa utoaji elimu kwa jamii kuhusu   afya ya akili kwa jamii,kwani inashirikisha  jamii katika utambuzi wakusimamaia tiba ya afya ya akili, kuwafikia walipo kwakuwapa uelewa ili wagonjwa watambuliwe mapema ili kupunguza wagonjwa pamoja na gharama za uendeshaji.


Kwa upande wao Daktari Suluma Aslani wa Hospitali yaTaifa ya  afya ya akili Mirembe ambaye pia anasomea udaktari bingwa wa afya ya akili  katika chuo Kikuu cha Dodoma ametoa wito kwa jamii kuwahi hospitali   mapema pale wanapoona dalili hizo  kwani ugonjwa huo unatibika huku Daktari Sadick Mandari akiiomba Serikali kufanya juhudi kubwa ya utoaji elimu  kwa jamii kuzuia magonjwa ya afya ya akili ambayo yamekuwa na athari mbalimbali ikiwemo vitendo vya mauaji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »