WAANDISHI WA HABARI WAPEWA ELIMU YA KILIMO MAONESHO YA NANENANE

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA  ELIMU YA KILIMO MAONESHO YA NANENANE

Na Barnabas Kisengi Dodoma Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma wanetembelea Banda la Dayosisi ya Tanganyika (DCT) kupatiwa elimu ya kilimo cha mazao na mbogamboga ili kuweza kupata elimu ya kilimo biashara. Akizungumza na wanahabari hao Afisa Kilimo kutoka Dayosisi ya Tanganyika (DCT) Bi SALOME KIMAMBO ameseme kilimo wanachofundisha wakulima wengi ni kilimo biashara kwakuwa unakuwa

Na Barnabas Kisengi Dodoma


Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma wanetembelea Banda la Dayosisi ya Tanganyika (DCT) kupatiwa elimu ya kilimo cha mazao na mbogamboga ili kuweza kupata elimu ya kilimo biashara.


Akizungumza na wanahabari hao Afisa Kilimo kutoka Dayosisi ya Tanganyika (DCT) Bi SALOME KIMAMBO ameseme kilimo wanachofundisha wakulima wengi ni kilimo biashara kwakuwa unakuwa na eneo dogo lakini unalima mazao mengi na yenye tija kwa wakulima wengi.


Bi SALOME KIMAMBO amesema DCT imekuwa ikitoa elimu kwa wakulima katika wilaya ya Dodoma Mjini, Chamwino na Bahi ambapo mpaka sasa zaidi ya wakulima elfu 25 wamesha patiwa elimu hiyo Katika wilaya hizo Mkoani Dodoma.
“Nimefurahi kuwaona nyinyi Waandishi wa Habari kuja kujifunza hapa swala la kilimo biashara kwa kuwa taaluma yenu ni kuelimisha jamii hapa natumaini mtaelimisha vizuri juu ya kilimo biashara kama mlivyojionee wenyewe katika eneo la shamba letu”Amesisitiza Bi Kimaro.


Aidha AFISA KILIMO huyo amewaambia Waandishi hao sasa imefika wakati nao wajishughulishe na shughuli za kilimo kwakuwa wana fursa kubwa ya kuweza kujiinua kiuchumi kwa kuwa na mashamba na kuweza kulima kilimo biashara.


Kwa upande wake Mwandishi wa Habari wa kituo cha EATV Danyel Mkate ameshukuru kupatiwa elimu ya kilimo biashara ambapo amesema wao kama Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma sasa wanatakiwa jifunza Kilimo na kuanza kujiwekeza katika kilimo biashara kwa kuna maisha mengine nje ya taaluma ya uandishi wa habari.


Waandishi wa habari waliopata elimu ya kilimo biashara katika maonyesho ya nane nane katika shamba Darasa la Dayosisi ya Tanganyika DCT ni Danyeli Mkate kutoka EATV, Neema Mzirai wa ABM Fm Redio, Mariam Tonge wa Uhuru fm Redio na Barnabas Kisengi wa J Five Blog.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »