Kilimo hifadhi kuwa mkombozi Kwa wakulima Mkoani Dodoma

Kilimo hifadhi kuwa mkombozi Kwa wakulima Mkoani Dodoma

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Kutokana na kuwepo kwa mvua kidogo na mtawanyiko na uharibifu wa Mazingira jambo ambalo hupelekea wakulima katika Mkoa wa Dodoma kupata mazao kidogo Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Jijini dodoma imekuja na Mpango wa Kilimo hifadhi ili kuwanusuru wakulima wa Mkoa wa Dodoma kuweza kulima kwa kisasa na kupata mazao mengi na

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Kutokana na kuwepo kwa mvua kidogo na mtawanyiko na uharibifu wa Mazingira jambo ambalo hupelekea wakulima katika Mkoa wa Dodoma kupata mazao kidogo Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Jijini dodoma imekuja na Mpango wa Kilimo hifadhi ili kuwanusuru wakulima wa Mkoa wa Dodoma kuweza kulima kwa kisasa na kupata mazao mengi na yenye tija kwa wakulima wa Mkoa wa Dodoma.


Akizungumza na J Five Blog Afisa kilimo na Mikopo kutoka Dayosisi Central Tanganyika (DCT)  SAMWELI ELINURU amesema kilimo hifadhi kimekuwa mkombozi kwa wakulima wengi Mkoani Dodoma kwa sababu kubwa tatu ambapo kutokana na Mkoa mzima wa Dodoma kuwa na mvua chache na mtawanyiko, uharibifu wa Mazingira na kuongezeka kwa watu kunafanya aridhi kupungu wao kama wataala walifanya tafiti ya kutosha na kujiridhisha na kuja na Mpango mkakati wa kuanzisha Kilimo hifadhi ambacho kimekuwa mkombozi kwa wakulima wa Mkoani Dodoma.
“Kutokana na Wananchi kuwa wanaongezeka matumizi ya aridhi ya maeneo ya Kilimo yamekuwa yakipungu na uharibifu wa Mazingira na kuwepo kwa mvua chache Mkoani Dodoma sisi kama wataalamu wa kilimo tulikuja na mkakati wa kilimo hifadhi ambacho kimekuwa mkombozi kwa wakulima wetu hapa Mkoani Dodoma tumekuwa tukiwapatia elimu katika maeneo yao huko vijijini na hapa katika maonyesho ya nane nane wakulima wengi wamejitokeza katika shamba Darasa letu kujifunza juu ya kilimo hifadhi na wengi wao wameelewa umuhimu wa kilimo hichi ambacho unakuwa na eneo dogo lakini ukilima kilimo hifadhi na mchanganyiko unalima kilimo chenye tija kwakuwa unapata mazao mengi kwa wakati mmoja”amesisitiza Be SAMWELI.


Kwa upandewake Meneja Tathimini na Ufutiliaji kutoka Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) LAURENCE LWONJI ameseme kuwa wao wanafanya ushawishi na uteuzi kwa wakulima wamekuwa wakishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima kulima kilimo hifadhi na kilimo chenye tija kwa wakulima.


Meneja Tathimini na na ufuatiliaji LWONJI ameseme wanapoanza mradi wamekuwa wakichukua taarifa ya mkulima alipokuwa akilima Kilimo cha mazoea mkulima akivuna mazao wamekuwa wakipata gunia tatu hadi nne kwa Kilimo cha mazoeya ambapo wanampatia elimu ya kilimo hifadhi na pindi anapovuna mkulima hupata gunia sita hadi saba katika hekari moja hapo ndio utaona tofauti ya Kilimo mazoea na Kilimo hifadhi kilivyo na umuhimu wake kwa wakulima wetu utaona sasa wanabadilika.


Naye AFISA KILIMO kutoka Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) SALOME KAMARO amesema katika sherehe za wakulima na wafugaji nane nane kanda ya kati yanayofanyika Katika viwanja vya nzuguni jijini Dodoma yameleta mwamko kwa wakulima wengi kufika katika shamba Darasa la Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) kujifunza juu ya Kilimo hifadhi ambacho wanekuwa wakiwaekimisha wakulima wengi katika eneo lao liliopo katika viwanja hivyo vya nane nane vilivyo nzuguni jijini Dodoma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »