Nathan Chibehe Aibuka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma

Nathan Chibehe Aibuka kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Nathan Chibehe ameibuka kuwa mshindi nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma baada ya kumshinda aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, Herry Kiwaya kufuatia chaguzi zinazoendelea kufanyika ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Jijini Dodoma uliofanyika katika Jengo la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi 

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Nathan Chibehe ameibuka kuwa mshindi nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma baada ya kumshinda aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, Herry Kiwaya kufuatia chaguzi zinazoendelea kufanyika ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Jijini Dodoma uliofanyika katika Jengo la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi  Kata kilimani Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini Said Kasote Amesema kuwa kura zilizopigwa ni kura 64 kura zilizoharibika ni kura 2 na kura halali ni kura 62.


Kasote amesema kuwa wagombea nafasi ya Mwenyekiti walikuwa ni Haruna Kifimbo alipata kura 1, Herry kiwaya alipata kura 27 na Nathan Chibehe ameibuka kuwa mshindi kwa kura 34 hivyo alimtangaza Nathan Chibehe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini JABIR SHEKIMWERI amewapongeza viongozi wote walio chaguliwa katika nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi kata ya kilimani huku akiwataka  viongozi hao kuwa uchaguzi umekwisha kama kulikuwa na makundi sasa yavunjwe na kubaki na kundi moja la CCM ili kuweza kukijenga chama.


Amebainisha kuwa kazi iliyopo ni kuijenga Chama na kukimarisha kwa kuwatumikia wanachama na Wananchi wa Kata ya kilimani.


Naye Mwenyekiti wa zamani wa chama Cha Mapinduzi kata ya kilimani Ndugu Herry kiwaya amewashukuru wajumbe na viongozi walio chaguliwa na kuwatakia majukumu mema ya utendaji wa kazi za Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani.


Mmoja wa Wajumbe waliochaguliwa  kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Nathan Chibehe amewashukuru wanachama kwa kumuamini na kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani na kuahidi kutoa ushirikiano nakuahidi kuvunja makundi yaliyokuwepo ili kujenga Chama.
“Sasa Mimi ndio Mwenyekiti wenu kuanzia sasa hivyo yale makundi yetu tuyavunje na kuwa na kundi moja tu la Chama cha Mapinduzi kama alivyotuasa Mjumbe wa Halimashauri ya Mkoa JABIR SHEKIMWERI hapa sasa kubwa ni kuimarisha Chama na kuhakikisha tunaongezea idadi ya wanachama na kuimarisha jumuiya zote kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani”Alisisitiza Mwenyekiti Nathan Chibehe

Hata hivyo Chibehe amewataka wanachama na viongozi mbalimbali kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi Agost 23 mwaka huu Ili serikali iweze kupata twakaimu sahihi ya watu na Makazi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »