Vijue Vivutio vya Utalii wa Ndani na Historia ya Nchi yetu ya Tanzania kabla ya kupata Uhuru Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma

Vijue Vivutio vya Utalii wa Ndani na Historia ya Nchi yetu ya Tanzania kabla ya kupata Uhuru Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma

Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma TANZANIA ni nchi yenye vivutio vya ndani Katika maeneo mengi ya mikoa na Wilaya zake hivyo yatupasa watanzania kupenda kufanya Utalii wa ndani ya nchi yetu na kuweza kufanya Utalii wa ndani huku pia tukijifunza historia ya nchi yetu kabla ya kupata Uhuru na baada ya kupata Uhuru. Nikizungumzia baadhi

Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma


TANZANIA ni nchi yenye vivutio vya ndani Katika maeneo mengi ya mikoa na Wilaya zake hivyo yatupasa watanzania kupenda kufanya Utalii wa ndani ya nchi yetu na kuweza kufanya Utalii wa ndani huku pia tukijifunza historia ya nchi yetu kabla ya kupata Uhuru na baada ya kupata Uhuru.


Nikizungumzia baadhi ya vivutio vya ndani ya nchi Wilayani Mpwapwa Mjini eneo la stendi ya mabasi utaukuta Mti mkubwa ambapo miaka ya 1850 Mti huu ulikuwa ukitumika kuwanyomgea watumwa waliokuwa wakitoka Mkoani kigoma na Tabora yani wakitokea bara kuelekea pwani bagamoyo walipita Wilayani Mpwapwa na wale watumwa walikuwa wakipumzika kwenye Mti huo na wale walioonekana wamechoka na hawana uwezo wa kuendelea na safari ya kwenda pwani waliweza kinyongwa katika Mti huo ambao hadi leo mwaka  2022 Mti huo Bado upo na inajulikana kwa jina la Mti Mkuu hivyo watanzania tunaweza kufika hapo kufanya Utalii wa ndani.


Aidha tukiachana na Mti huo kuna kisima kirefu nyuma ya stendi ya mabasi kisima hicho nacho kilitumika na watumwa hao kutoka bara wakielekea pwani hapo walifika na kuweza kunywa Maji na kuoga kabla hawajaendelea na safari ya kuelekea pwani  na watumwa walikuwa wakipumzika sana Wilayani Mpwapwa ambapo hadi walifanikiwa kujenga kanisa la Anglican church katika eneo la ving’awe Wilayani Mpwapwa miaka hivyo ya 1852 hivi vyote vivutio vya Utalii wa ndani na historia vinapatikana Wilayani Mpwapwa.


Pia kuna josho la kwanza la Africa Mashariki na kati josho hilo la kwanza kujengwa limejengwa 1905 Katika eneo la kikombo ambapo sasa kuna kituo cha utafiti wa mifugo hivyo vyote ni Utalii wa ndani na historia ya nchi yatu.


Pia kunakijimto kijulikanacho kama moto kikombo huu unatabia ya kutiririsha maji mwaka mzima na Katika moto huu mtunzi mkubwa wa mashairi hapa nchini amekuwa akitumgia mashairi yake mengi na sii mwingine ni Ndugu SHABAN ROBAT amekuwa akitumia muda wake mwingi kutunga mashairi yake Katika mto huo wa kikombo.
Watanzania twapaswa kuwa na tabia ya kufanya Utalii wa ndani ya nchi yetu ili tuweze kujifunza pia historia ya nchi yatu tuliko toka tuliko Sasa na tuendako ili kuwaeza kuwaachia watoto Wetu historia ya nchi sasa fika Wilayani Mpwapwa uweze kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria na Utalii wa ndani.


Aliyewaandalia makala hii fupi ya kuvutia ya Utalii wa ndani na historia ya nchi yetu enzi za watumwa ni Mimi Mwandishi Mwandamizi nguli Barnabas Kisengi kutoka Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma Nchini Tanzania kwa mawasiliano zaidi ni Email bksengi@gimail.com mobile 0622-846262. 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »