MRADI WA BWAWA LA MAJI MEMBE – CHAMWINO, UTAKAOGHARIMU TSH. 11.965 Bln. KUANZA HIVI KARIBUNI

MRADI WA BWAWA LA MAJI MEMBE – CHAMWINO, UTAKAOGHARIMU TSH. 11.965 Bln. KUANZA HIVI KARIBUNI

Ña Mwandishi Wetu Chamwino Akikabidhi mradi wa ujenzi wa bwawa la maji  la Membe, mradi utakaogharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 11.965  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Gift Msuya amesema, mara bwawa hili litakapokamilika litawezasha umwagiliaji wa hekari 8000.Bwawa litakuwa na maji kwa mwaka mzima.Msuya, ametoa shukrani za dhati  kwa RAIS SAMIA SULUH HASSAN  Kwa kuongeza


Ña Mwandishi Wetu Chamwino


Akikabidhi mradi wa ujenzi wa bwawa la maji  la Membe, mradi utakaogharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 11.965  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Gift Msuya amesema, mara bwawa hili litakapokamilika litawezasha umwagiliaji wa hekari 8000.Bwawa litakuwa na maji kwa mwaka mzima.
Msuya, ametoa shukrani za dhati  kwa RAIS SAMIA SULUH HASSAN  Kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo.
Aidha Msuya amemshukuru Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kwa kuridhia fedha hizi zije kwenye mradi wa bwawa la maji la Membe. 

Mradi huu ulisanifiwa mwaka 2016 lakini kwa kipindi chote chote hicho haukutekelezeka hadi mwaka huu ambapo utaanza 01/9/2022 na kukamilika 01/9/2023.Miradi huu ukikamilika  Wilaya ya Chamwino tutakuwa na chakula cha kutosha. 
“Ombi langu kwa Wanamembe ni kutoa ushirikiano katika mradi huu kwani ni wenu. Ombi kwa Mkandarasi kutekeleza mkataba kwa wakati na kwa viwango na makabaliano ya mkataba”Alisisitiza Msuya.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Bi AZIZA MUMBA amesema ni furaha  sana kuupokea mradi huu  tumepewa upendeleo wa hali ya juu  maana kuna halmashauri nyingi nchini lakini Mkoa wa Dodoma umepata fursa hii adhimu. 


Bwawa la maji la Membe litakuwa mkombozi kwa uchumi wa wananchi wa Dodoma, na litapunguza changamoto za ajira kwa vijana kwani watazalisha chakula mara 3/4 kwa mwaka.

 
Mkoa utakuwa karibu sana kwenye usimamizi.Wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kuna kazi za elimu na za mikono hii hela ibaki hapa Membe na Mkoani Dodoma,wananchi wawe tayari kufanya kazi hizo.


Meneja wa Mradi Eng.Raphael Laizer, ameeleza kuwa watachimba  tuta lenye kina cha 451 m, Upana 12  na kimo cha  110-117m hii ni kulingana na hali halisi .Mradi huu utakamilika ndani ya miezi 12. Kutakuwa na sehemu ya mifugo na matoleo ya maji ya kunywa ya watu.


Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Tume ya umwagiliaji Mhandisi mkazi Eng. Salehe Ramadhani ameeleza kuwa Bwawa la Membe litakuwa na ukubwa. wa 5.1mln cubic meters.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »