AIS DK.MWINYI AMEMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA ZAECA

AIS DK.MWINYI AMEMUAPISHA MKURUGENZI MKUU WA ZAECA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuhakikisha anaanza kazi mara moja kufanya uchunguzi wa ripoti ya CAG kwa wale wote waliobainika kuiba fedha za umma na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Dk. Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuhakikisha anaanza kazi mara moja kufanya uchunguzi wa ripoti ya CAG kwa wale wote waliobainika kuiba fedha za umma na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo mara baada ya kumuapisha Mkurugenzi huyo na kumkabidhi ripoti hiyo hafla iliyofanyika Ikulu jijini Unguja.

Alisema anamkabidhi ripoti hiyo kuhakikisha anaifanyia kazi vya kutosha ambalo ni jukumu lake la kwanza na angependa kuona katika maeneo yote yaliyooneshwa kuwa na kasoro basi uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa.

Dk. Mwinyi alisema ni wakati sasa kwa ZAECA kutimiza wajibu wake huo kwani sio vizuri kila mwaka wanapokea ripoti ya CAG alafu hakuna taarifa za utendaji wa ZAECA juu ya yale yaliyoonekana ni kasoro dhidi ya yale wote yaliyosemwa.

“Hatusemi kwamba yote yanayotendwa kwamba hayana majibu tunasema ni jukumu la chombo hichi inapata majibu na kuondoa hoja hizo kupitia kwa CAG na wale wanaothibitika kwamba wamefanya wizi au uhujumu wa uchumi basi lazima ionekane wanapelekwa katika vyombo vya kisheria.

Alisema ripoti hiyo ilisema wazi kuna baadhi ya maeneo ikiwemo ZRB watu wamekuwa wakipokea fedha za kodi zinazolipwa na walipa kodi na wanapewa risiti za bodi hiyo lakini fedha haziingii katika akaunti ya ZRB anataka uchunguzi wa kina kuona kila aliehusika na hilo atambulike na hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake.

Alimuahidi kumpa majina ya watu ambao walimtumia sms kwamba wao walilipa ZRB na risiti wanazo na sasa wanadaiwa tena kwa kuwa fedha hazikufika katika bodi hiyo kwani mchezo huo ni wa siku nyingi na lazima utafutiwe ufumbuzi ili usiendelee.

Eneo jengine alisema ni Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi ambapo kuna fedha taslim zilipelekwa kwenye kampuni ambazo hazipo na hazina usajili haiwezekani na hata kwa Wizara ya Afya ikawa basi ni lazima fedha hizo zipatikane na wahusika wachukuliwe hatua stahiki.

Hata hivyo alimtaka Mkurugenzi huyo kutoishia katika ripoti hiyo pekee kwani zipo taarifa nyingi nje ya CAG za ubadhilifu na wizi wa mali za umma angependa kupata majibu.

Alisema tasisi nyingi zimekuwa hazitoi taarifa za utendaji hivyo angependa kuona kuna utofauti katika utendaji wa tasisi hiyo na kuona kila baada ya muda wanatoa taarifa juu ya utendaji wao hadharani ili kujua hatua zilizochukuliwa, watu wangapi wameshitakiwa, kesi zilizoshinda, zilizoshindwa na kesi zilizokosa ushahidi na kuondolewa.

Alisema mambo hayo ni muhimu katika kutafuta haki kwani yanayosemwa kuwa kila aliyetuhumiwa ana kosa hivyo angependa kuona wale wote ambao hawana makosa basi hawaishi katika woga na kuwaambia hawana makosa wapo huru na haki ipatikane.

“Vyombo vya sheria ikiwemo DPP na mahakama zetu ni lazima kufanya kazi ya ziada ili kukomesha wizi, ubadhilifu wa mali za umma haya mambo yakiachiwa kuendelea hatutoweza kufanya yale tuliyowaahidi wananchi kwani tumewaahidi mengi ambayo yanahitaji rasilimali na kama zinaingia katika mifuko ya watu na hatuchukui hatua tutashindwa kuyatekeleza hayo,”

Alisema kwake ni suala hili ni muhimu na ndio maana anataka mabadiliko katika utendaji wa chombo hicho pamoja na vyombo vyengine ambavyo vitasaidia kufikia azma ya serikali ya kuondoa hali hiyo katika jamii,” alisema.    

Alisema wakati anapokea ripoti ya CAG alionesha wasiwasi wake juu ya utendaji wa ZAECA jambo ambalo lilipelekea kujiuzulu kwa mkurugenzi aliyekuwepo akiwa anatekeleza uwajibikaji.

“Nilivyosema ZAECA wakajitathmini nilikuwa naonesha kutoridhika kwangu na utendaji wa chombo hicho,” alisema.   

Alisema lengo lake ni kuonesha matarajio aliyonayo kwa chombo hicho

Rais Mwinyi alisema katika nchi za kidemokrasia kunakuwa na vyombo vinavyotazama utendaji ikiwemo chombo cha CAG. Baraza la Wawakilishi, Mabaraza ya Madiwani na vyombo vya habari ambao hueleza mambo ambayo hayatakiwi kufanyika ndani ya serikali ili serikali iweze kuchukua hatua,” alisema.

Alibainisha kwamba serikali inapopata mambo hayo ina wajibu ya kuyafanyia utafiti wa kutosha na hatiame kuchukua hatua za kisheria na jukumu kubwa linakwenda kwa chombo cha ZAECA.

Alibainisha kwamba ili aweze kufanya hivyo ni lazima kuwa na ushirikiano wa kutosha na Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kupata matokeo.

Alitumia nafasi hiyo kuiagiza Ofisi ya DPP kutekeleza wajibu wake ili kuweza kupata matokeo.

Alisema katika serikali yanapojitokeza matatizo hayo alafu hatua zisichukuliwe basi wanatoa mwanya kwa watu kufanya wanavyotaka kila mwaka na hawatoendelea kuzuia watu kuiba na kuendelea kufanya ubadhilifu wa mali za umma.

Dk. Mwinyi alisema imefika wakati sasa mtu kutambua kwamba ukichukua mali ya umma basi zipo hatua utakazochukuliwa na hayo ndio anayotaka kuyaona kwa chombo hicho.

Alimsisitiza Mkurugenzi huyo kuhakikisha akafanye kazi kuhakikisha wale wote waliohusika basi wanabainika na wanachukuliwa hatua.

Mbali na hayo alisema ni lazima kuongeza uwezo wa chombo hicho kufanya kazi na kuhakikisha kuna watu wenye ueledi unaotakiwa ili kuweza kupata matokeo mazuri.

“Hiyo ni kazi pia ambayo tunakukabidhi uweze kuijenga ZAECA na serikali itakusaidia kufanya hivyo lakini lazima tuwe na chombo ambacho kitaweza kufanya kazi bila ya kusita,” alibainisha.

Rais Mwinyi aliahidi kwamba serikali itahakikisha inampa kila aina ya msaada ili aweze kutimiza wajibu wake na kumsisitiza kufanya kazi na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama ili kupata mafanikio mazuri.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Ali Abdalla Ali, aliahidi kwamba yale yote aliyoagizwa ni wakati wake sasa kwenda kuyafanyia kazi kwa nguvu zote na zaidi kuchukua hatua kama anavyotaka kiongozi wa nchi.

“Rais anataka kuona hatua zinachukuliwa lakini kwa kuzingatia haki na misingi ya uadilifu na hicho ndicho ambacho kikubwa tutakiangalia hasa kwa kuanzia na ripoti ya CAG na maeneo mengine yote ambayo yanaonesha kwamba kuna ubadhilifu lengo ni kuona fedha za umma, matumizi ya fedha zinatumika vizuri kwa maslahi ya watu wote,” alibainisha. Alitumia nafasi hiyo kumshuru Rais Mwinyi kwa kumteuwa na kumuamini kuweza kumsaidia na wananchi wa Zanzibar kuona masuala ya wizi na uhujumu uchumi yanafanyiwa kazi na hatua zinachukuliwa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »