BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA

Ña Barnabas Kisengi Dodoma Muswada wa sheria ya Usimamizi wa maafa Imepitishwa bungeni leo jijini Dodoma baada ya kuwasilisha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene  alisema  kupitishwa kwa muswada huo  kutawezeshwa kutungwa . Waziri Simbachawene  amesema katika kipindi cha miaka saba ya utekelezaji wa sheria ya maafa

Ña Barnabas Kisengi Dodoma

Muswada wa sheria ya Usimamizi wa maafa Imepitishwa bungeni leo jijini Dodoma baada ya kuwasilisha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene  alisema  kupitishwa kwa muswada huo  kutawezeshwa kutungwa .


Waziri Simbachawene  amesema katika kipindi cha miaka saba ya utekelezaji wa sheria ya maafa sura ya 242 na kanuni zake za mwaka 2017 kumekuwa na mafanikio mbalimbali yakiwemo kuanzishwa kwa Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa majanga na kuratibu dharura nchini.


Waziri Simbachawene amesema kuwa mafanikio mengine ni Kuboresha utabiri wa hali ya hewa, Kuanzishwa kwa Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania na Kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa na kufanya ufuatiliaji wa ugawaji wa misaada hiyo kwa waathirika.


“ Pia  Ofisi  ya Waziri Mkuu imefanikiwa kusimamia maghala sita ya kikanda ya kuhifadhi misaada ya kibinadamu, Kuanzishwa na kujengewa uwezo kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa za ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji au Mtaa kupitia mafunzo, Kuelimisha, kuhamasisha na kuwawezesha wadau wa maafa kuhusu kuzuia, kujiandaa, kukabili maafa na kurejesha hali baada ya maafa kutokea kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya vyombo vya habari,”amesema Waziri Simbachawene.


Pia akizungumzia  Sheria inayopendekezwa kutungwa alieleza kwamba  inalenga kuweka mfumo wa kusimamia maafa kuanzia hatua za kuzuia na kupunguza madhara ya majanga, kujiandaa, kukabili na kurejesha hali endapo maafa yanatokea kwa kuzingatia sera, sheria na miongozo.


“Muswada unajikita katika kuimarisha uwajibikaji wa kila sekta na jamii pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza afua za usimamizi wa maafa katika ngazi zote ili kuimarisha ustahimilivu kwa maendeleo endelevu,”alieleza.


Katika hatua nyingine waziri alifafanua kuwa “Muswada unapendekeza kufutwa kwa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Sura ya 242 na kupendekeza itungwe Sheria mpya ambayo itaimarisha mfumo wa usimamizi wa maafa nchini kwa kuondoa changamoto za Sheria iliyopo sasa,” alifafanua Mhe. Simbachawene.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »