Na Mwandishi Wetu Mbeya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bahati Geuzye amesisitiza umuhimu wa watendaji wa Halmashauri nchini kushirikiana na TEA katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu inayofadhiliwa na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA katika maeneo yao ili itekelezwe kwa ufanisi. Mkurugenzi mkuu wa TEA amesema
Na Mwandishi Wetu Mbeya
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bahati Geuzye amesisitiza umuhimu wa watendaji wa Halmashauri nchini kushirikiana na TEA katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu inayofadhiliwa na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA katika maeneo yao ili itekelezwe kwa ufanisi.
Mkurugenzi mkuu wa TEA amesema hayo wakati akitoa wasilisho katika Mkutano Mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) unaofanyika jijini Mbeya.
Bi Bahati Geuzye amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha Sh.bilioni 8.9 zimetengwa kwa ajili ya kufadhili miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sehemu mbali mbali nchini.



Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu na miudombinu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *