MWILI WA ALIYEKUWA AFISA HABARI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ‘MAGENI ZUMBI’ WAAGWA JIJINI DODOMA

MWILI WA ALIYEKUWA AFISA HABARI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI ‘MAGENI ZUMBI’ WAAGWA JIJINI DODOMA

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi HAMADI MASAUNI ameingoza  kuagwa kwa mwili wa Marehemu Mageni Zumbi aliyekuwa Afisa Habari Daraja II katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyefariki dunia sempetemba12 , 2022 kwa  ajali ya Gari katika eneo la chimala wilaya Mbarali Mkoani Mbeya. Waziri Mhandisi HAMADI MASAUNI amesema

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi HAMADI MASAUNI ameingoza  kuagwa kwa mwili wa Marehemu Mageni Zumbi aliyekuwa Afisa Habari Daraja II katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyefariki dunia sempetemba12 , 2022 kwa  ajali ya Gari katika eneo la chimala wilaya Mbarali Mkoani Mbeya.


Waziri Mhandisi HAMADI MASAUNI amesema Marehemu Mageni Zumbi alikuwa mchapakazi hodari katika Wizara yake na alikuwa Binti Pole na mnyenyekevu na aliyekuwa anapenda kujifunza kila siku katika utendaji wake wa kazi.


Naye Naibu Waziri Ofisini ya Makamu wa RAIS Muungano na Mazingira HAMISI HAMZA CHILO ambaye awali akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema alifanya kazi vizuri na Marehemu Mageni Zumbi na wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho.
“Jana nilitoka kwenye kikao cha Bunge dereva wangu alinipa taarifa hiyo hakika nilihuzunika Sana kwakuwa ni mtu niliyemfahamu na kufanya naye kazi kwa karibu Sana” amesema Naibu Waziri Chilo.


Naibu Waziri HAMZA CHILO amewataka ndugu na jamaa kuendelea kumwombea Katika Sala pia amewaambia Waombolezaji kujianda Katika maisha ya hapa Duniani kwani kuna maisha mengine baada ya kifo.


Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi CHRISTINA MWANGOSE  amesema kuwa wamepata pengo kubwa katika kitengo Cha habari kwakuwa Marehemu Mageni Zumbi alikuwa mchapakazi na alikuwa akijituma Katika kazi.
“Nilikuwa nafanya kazi kwa ukaribu Sana na Marehemu Mageni Zumbi alikuwa akiheshimu kila mtu na alitumia muda Wake mwingi kujifunza hata kabla ya umauti kumfika alitoka Safari na alipo fika ofisini aliniamba yote uliyo nifundisha nimeyaelewa bado moja tu sasa hili kwakuwa nina Safari ya mbeya nikirudi utanifundisha aliongea Marehemu Mageni Zumbi….hivyo tumepata pengo kubwa katika kitengo cha Habari hapa wizarani”alisema Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano wizara ya mambo ya ndani .


Awali akisoma wasia wa Marehemu Mageni Zumbi Afisa Habari Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Felix Mwagara amesema Marehemu Mageni Zumbi alizaliwa February 16,. 1993 alimaliza Elimu ya shule ya msingi mwaka 2006, secondary 2010 na chuo kikuu Dar es Salaam 2013 na sempetembar 01  2020 alipata kazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na sempetembar 01 2021 alisibitisha kazi.


Ibada ya kuanga mwili wa Marehemu Mageni Zumbi ilifanyika katika kanisa kuu la KKKT Jijini Dodoma ambapo mchungaji akiwataka Waombolezaji kuhakikisha wanakuwa na tabia ya kutenga muda wa kwenda kwenye ibada na pia waakikishe wamejiandaa kila wakati kwani kifo hakina muda wala saa kubwa ni kujianda Kila wakati.


Ibada ya kumwaga mpendwa wetu Marehemu Mageni Zumbi uliuzuriwa na viongozi Mbalimbali wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, Maafisa Habari wa Wizara Mbalimbali na Waandishi wa Habari Mkoani Dodoma na Wananchi wa Mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani alikokuwa aliishi Marehemu Mageni Zumbi.
 Mwili wa Marehemu Mageni Zumbi umesafirishwa kuelekea Mkoani Kilimanjaro Wilayani Hai boma la ng’ombe kesho saa nane mchana ambapo utapumzishwa Katika nyumba yake ya Milele kesho Sempetemba 15, 2022 Mazishi hayo yataongozwa na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi JUMANNE SAGINI.Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »