WATU 54 WATHIBITIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA SURUA NCHINI

WATU 54 WATHIBITIKA  KUWA NA MAAMBUKIZI YA  UGONJWA  WA SURUA NCHINI

Ña Barnabas Kisengi Dodoma Wizara ya Afya Imethibitisha kuwa watu 54 wamekutwa na maambukizi ya ugonjwa wa surua kwa kipindi cha julai hadi agosti 2022 hapa Nchini huku wakiwemo wagonjwa 48 waliokuwa na umri usiozidi miaka 15 na wagonjwa 6 waliokuwa na umri wa zaidi ya  miaka 15 huku kukiwa hakuna taarifa ya kifo kilichobainishwa

Ña Barnabas Kisengi Dodoma


Wizara ya Afya Imethibitisha kuwa watu 54 wamekutwa na maambukizi ya ugonjwa wa surua kwa kipindi cha julai hadi agosti 2022 hapa Nchini huku wakiwemo wagonjwa 48 waliokuwa na umri usiozidi miaka 15 na wagonjwa 6 waliokuwa na umri wa zaidi ya  miaka 15 huku kukiwa hakuna taarifa ya kifo kilichobainishwa mpaka sasa.


Waziri wa afya  Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa kwa umma kuhusu ongezeko la ugonjwa wa surua hapa Nchini.


 Waziri Ummy amesema kuthibitisha ugonjwa huo wizara inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa wahisiwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa na tetesi katika ngazi ya jamii,kutumia timu ya wataalamu  kwenda maeneo yaliyoathirika kwa  wagonjwa wengi na kutoa elimu kwa watoa huduma za afya na jamii kwa ujumla kuhusu dalili na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo.

“Dalili kuu za ugonjwa wa surua ni homa na vipele, inayoweza kuambatana na kikohozi, mafua,macho kuwa mekundu na vidonda mdomoni, aidha amesema ugonjwa huo usipo dhibitiwa mapema unaweza kuleta madhara katika masikio au kusababisha homa ya mapafu, upofu wa macho, homa ya uti wa mgongo na kupelekea kupoteza maisha” amesema Ummy.
“Uchunguzi wa majibu ya vipimo Toka mahanara ya taifa ya afya umeonyesha kuwa halmashauri Saba zimekizi vigezo vyakuwa na mlipuko wa ugonjwa wa surua, ambapo wagonjwa 38 wamethibitika katika halmashauri za bukoba sampuli 3, handeni sampuli 4, kilindi sampuli 3, mkuramga sampuli 4, manispaa ya kigamboni sampuli 8, manispaa ya temeke sampuli 12, na  manispaa ya ila sampuli 4” amesema Ummy.


Pia waziri Ummy amesema imebainishwa kuwa zaidi ya watoto 40, 000 wenye umri chini ya miaka 5 hawajapata chanjo, mikoa ambayo watoto awajapata chanjo ni kigoma, Kagera, mara, songwe, manyara na mbeya na mikoa ambayo watoto hawaja kamilisha chanjo ni Tabora , Dar es salaam, Arusha, Geita, Rukwa, shinyanga, Manyara, Pwani, Singida, Ruvuma, Dodoma, kigoma, Morogoro, Lindi, songwe,Mtwara, Katavi na mbeya.
” Sababu zinazotajwa kuathiri utoaji wa chanjo ni janga la uviko 19. Sababu hii aijaathiri Tanzania Bali inchi nyingi duniani,” amesema Ummy.


Hivyo ametoa rai kwa umma kupeleka watoto kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya ili wapatiwe chanjo ya surua au Rubella kulingana na umri wao huku akitoa ufafanuzi wa chanjo ya surua au rubella hutolewa kwa watoto wanapofikia umri wa miezi 9 kwa dozi ya kwanza na miezi 18 kwa dozi ya pili ili kupata kinga kamili.


Waziri Ummy ameagiza waganga wakuu wa Mikoa na halmashauri zote nchini kuchuka hatua za kufatilia wagonjwa waliothibitika katika maenel yaliyoathirika, kuimarisha uduma za matibabu kwa wagonjwa wye dalili za surua pamoja na kuimarisha huduma za uchanjaji kwa watoto waliofikia umri wa kuchanja chanjo ya surua Kaa dozi zote mbili.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »