SERIKALI YAZITAKA HALMASHAURI KUANISHA MAENEO YA KIMKAKATI UJENZI WA VITUO VYA AFYA

SERIKALI YAZITAKA HALMASHAURI KUANISHA MAENEO YA KIMKAKATI UJENZI WA VITUO VYA AFYA

Asila Twaha, OR – TAMISEMI Serikali imezielekeza Halmashauri zote nchini kuanisha maeneo ya kimkakati ili ujenzi wa vituo vya afya vijengwe katika maeneo hayo na kurahisisha  upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia Afya Mhe.Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali bungeni leo  kwa

Asila Twaha, OR – TAMISEMI


Serikali imezielekeza Halmashauri zote nchini kuanisha maeneo ya kimkakati ili ujenzi wa vituo vya afya vijengwe katika maeneo hayo na kurahisisha  upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia Afya Mhe.Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali bungeni leo  kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Raia TAMISEMI wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu Mhe. Kiswaga aliyetaka kujua lini Serikali itapeleka huduma ya vituo vya afya katika vijiji vya Lutale, Kwamanga  na Igogo.


Waziri Dugange ameongeza kuwa Serikali ilishatoa utaratibu na kuzielekeza Halmashauri zote nchini kuanisha Kata za kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa  vituo vya afya.


Ameongezea kuwa  ujenzi wa vituo vya afya utazingatia vigezo na si kila eneo litajengwa vituo hivyo. 
Aidha, ametoa wito kwa Mhe. Mbunge  na Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya Magu kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuangalia na kuanisha maeneo yenye vigezo hivyo ili hatua za haraka zichukuliwe ujenzi uanze na  wananchi wapate huduma.


Naibu Waziri amewatoa hofu Waheshimiwa Wabunge kuwa, ujenzi wa vituo vya afya vitakavyojengwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa tiba amesema, bajeti ya mwaka 2022/23 Serikali imetenga  sh. bilioni 69.95 ambapo vifaa hivyo vitaenda  kwenye vituo vya afya 530 vinavyojengwa  nchi nzima.
“Ninapokea shukrani za Mbunge wa  Rungwe Mhe. Antony Mwantona kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluh Hassan kwa kujenga vituo vya afya vitatu ndani ya mwaka mmoja ndato,kimwa, imenjora” amesema Waziri Dugange.


Aidha ameongeza kuwa, vituo vya afya vilivyokamilika vitapewa kipaumbele kwa kupatiwa vifaa tiba ili viweze kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma.
Waziri Dugange amesema, Serikali itaendelea kusimamia sekta ya afya na kuendelea  kuweka mipango mizuri ili vituo vyote vinavyojengwa kuwekewa vifaatiba.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »