RAIS SAMIA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA KKKT, CHAMWINO IKULU

RAIS SAMIA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA KKKT, CHAMWINO IKULU

Na Mwandishi Wetu-Chamwino RAIS SAMIA SULUH HASSAN ametoa Tsh. Milioni 50 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chamwino Ikulu, kama ahadi ya mchango wake kwenye ujenzi unaoendelea wa Kanisa hilo.Akikabidhi Hati ya malipo hayo yaliyofanyika kwa njia ya Benki Mkuu wa mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule  ambae alimwakilisha RAIS SAMIA SULUH

Na Mwandishi Wetu-Chamwino


RAIS SAMIA SULUH HASSAN ametoa Tsh. Milioni 50 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chamwino Ikulu, kama ahadi ya mchango wake kwenye ujenzi unaoendelea wa Kanisa hilo.
Akikabidhi Hati ya malipo hayo yaliyofanyika kwa njia ya Benki Mkuu wa mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule  ambae alimwakilisha RAIS SAMIA SULUH HASSAN kwenye  ibada  Kanisani hapo, ameelezea Mhe. Rais ametoa mchango wake kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa Harambee ya Ujenzi iliyofanyika Agosti 28, 2022.
” Mhe Rais ametoa kiasi hicho kwakuwa ni Kiongozi mwenye hofu ya Mungu, pili Kanisa hili ni majirani zake kwani mpo karibu na Ikulu hivyo ametaka kuongeza ujirani wa Kiimani.

Tatu Mhe. Rais ameweka hazina yake Mbinguni kwa Mungu mahali ambapo haitaoza na Nne , Mhe. Rais anampenda kuona kila mtu anapata haki ya kuabudu sehemu iliyo salama ili mradi tu haivunji Sheria za nchi”.Amesema Mhe. Senyamule.


Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino  Gift Msuya amesema Harambe iliyofanyika kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo, imekua na mafanikio makubwa kwani ahadi mbalimbali za viongozi zilitolewa na zinatarajiwa kuwasilisha kwa Kanisa mwisho wa mwezi Septemba pia ameahidi kushughulikia suala la eneo la wazi ambalo limetolewa na msamaria mwema kwa ajili ya upanuzi wa Kanisa lakini kuna sintofahamu zimejitokeza kukwamisha makabidhiano ya eneo hilo.


Akitoa shukrani zake kwa niaba ya Kanisa, Askofu wa wa Kanisa hilo Bw. Amoni Kinyunyu, amemshukuru sana Mhe Rais kwa sadaka aliyoitoa na kumuahidi kwamba wataendele kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Kanisa linakamilika.
“Tunamuahidi Rais kwamba hatutabweteka kwa mchango huu bali tutaendelea na juhudi za kuchangisha michango zaidi kufanikisha kukamilisha hili kwani umoja wetu ndio nguvu yetu” Askofu Kinyunyu.


Ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Chamwino Ikulu ulianza mwezi Aprili mwaka huu baada ya kuona kuna uhitaji wa jengo kubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya waumini ambapo kwa Sasa wapo 400 , jengo hilo litakua na uwezo wa kuchukua waumini 600 hadi 800. Ujenzi wake unatarajiwa kugharimu kiasi cha Shilingi 326,677,500 na linatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »