WAZIRI WA MASAUNI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

WAZIRI WA MASAUNI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni (Mb), kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 2 cha Amri ya Uanzishwaji wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali ya Magereza, iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022 (The Prisons Corporation Sole Board (Establishment)(Ammendment) Order, 2022), amewateua Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe 10 wa Bodi ya Shirika

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni (Mb), kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 2 cha Amri ya Uanzishwaji wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali ya Magereza, iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2022 (The Prisons Corporation Sole Board (Establishment)(Ammendment) Order, 2022), amewateua Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe 10 wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA).

Waziri Masauni amemteua Inspekta Jenerali wa Polisi (Mst), Said Ally Mwema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza. Pia, amemteua  Bw. Moremi Marwa, kuwa Katibu wa Bodi hiyo.

Aidha, Waziri Masauni amewateua  Wajumbe wa Bodi hiyo kama ifuatavyo:-

  1. Bw. Emmanuel Akunay – Mjumbe
  2. Bw. Fuad Jaffer – Mjumbe
  3. Bw. Isaack Mazwile – Mjumbe
  4. Bw. Salim Aziz Salim – Mjumbe
  5. Mhandisi Theofilo Bwakea – Mjumbe
  6. Bi. Wanja Mtawazo – Mjumbe
  7. ACP John Itambu – Mjumbe  
  8. Bw. Raymond William Mndolwa – Mjumbe
  9. Bw. Revocatus Rachel – Mjumbe
  10.  Bi. Fatma Mangunda – Mjumbe

Uteuzi huo umeanza tarehe 20 Septemba, 2022.

Imetolewa na:-

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »