MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MSAGALI – MPWAPWA WAKABIDHIWA RASMI

MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MSAGALI – MPWAPWA WAKABIDHIWA RASMI

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amekabidhi kwa Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya mradi wa ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Chunyu kilichopo Kata ya Chunyu Wilaya ya Mpwapwa. Ujenzi wa Bwawa hilo umekabidhiwa kwa Mkandarasi anayefahamika kwa jina la Injinia Emmanuel Charles Mponda, chini ya kampuni

Na Barnabas Kisengi-Mpwapwa


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amekabidhi kwa Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya mradi wa ujenzi wa Bwawa litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Chunyu kilichopo Kata ya Chunyu Wilaya ya Mpwapwa.


Ujenzi wa Bwawa hilo umekabidhiwa kwa Mkandarasi anayefahamika kwa jina la Injinia Emmanuel Charles Mponda, chini ya kampuni ya GNMS Contractors Co. LTD ambaye ni ya Mzawa wa Tanzania.


Senyamule, ameongea na wanachi wa Chunyu kwenye mkutano wa hadhara, amewataka kulinda mazingira hasa ya Bwawa hilo kwani lina faida nyingi sana kwao.
” Bwawa hili litakapokamilika litakua na faida nyingi sana kwa nyinyi wakazi wa hapa kiuchumi kwani mutaweza kufanya kilimo cha kisasa pamoja na biashara na kujiongezea kipato”


Hata hivyo,  Senyamule hakusita kutoa shukrani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Bilioni 27 kwa ajili ya Ujenzi huo huku akisema;
“Rais ametoa fedha hizo kwa kuwathamini wananchi wa Chunyu na shida zao na Kwa kuwa ameamua kufanya mapinduzi makubwa kwenye kilimo ili Wakulima wa Tanzania wafanye kilimo cha kisasa na si cha kusubiri msimu wa mvua”.


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mwalimu Josephat Maganga, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiona Mpwapwa katika kuwekeza mradi huo mkubwa wa Bwawa la umwagiliaji na ametangaza vita na wote watakaobainika kufanya uharibifu wa mazingira kwa namna yoyote ile.


Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Malima naye amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Shilingi Bilioni 27 kwa ajili ya Ujenzi wa Bwawa hilo kwani hali ya Uchumi wa wakazi wa Chunyu majirani zao inakwenda kubadilika.
“Bwawa hili litakapokamilika, litakwenda kubadilisha Uchumi wenu pamoja na wa Vijiji jirani hivyo mna dhamana ya kusimamia ujenzi huu na kuhakikisha unakamilika kama ilivyokusudiwa ili kuleta thamani ya fedha hii iliyotolewa na Serikali” Amesema Mhe. Senyamule.  


Ujenzi wa Bwawa la Msagati ulianza kufanyiwa utafiti miaka 10 iliyopita na ujenzi wake unatarajiwa kuanza punde baada ya makabidhiano haya rasmi na utatumia kipindi cha miezi 18 mpaka kukamilika. Bwawa linatarajiwa kutumia eneo la ukubwa wa Hekta 3500, litabeba ujazo wa Lita Trilioni 90 za maji na maji hayo yanatarakiwa kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa mwaka mzima, kunyweshea mifugo pamoja na matumizi ya kawaida ya nyumbani isipokua kunywa.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »