WAVUNAJI MKAA WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UVUNAJI MKAA

WAVUNAJI MKAA WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA UVUNAJI MKAA

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma Serikali imewataka wananchi wanaofanya biashara ya mkaa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kwa kuwa kumekuwepo na wimbi la uvunaji wa mazao ya misitu, ukataji na uchomaji wa mkaa bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia biashara hiyo. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  Mary Masanja amesema hayo Bungeni jijini Dodoma kwa niaba

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma


Serikali imewataka wananchi wanaofanya biashara ya mkaa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kwa kuwa kumekuwepo na wimbi la uvunaji wa mazao ya misitu, ukataji na uchomaji wa mkaa bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia biashara hiyo.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  Mary Masanja amesema hayo Bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Nicodemus Maganga  Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
Amesema uvunaji holela wa mkaa umesababisha kutoweka kwa kasi kwa maeneo ya misitu na hatimaye kujitokeza kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi. 
Kuhusu kauli ya Serikali juu ya askari wa Misitu wanaopiga na kuwanyang’anya mkaa wananchi wa Mbogwe,  Mhe. Masanja amesema Wizara haitosita kuwachukulia hatua watumishi wake wanaohusika na uvunjaji huo wa sheria, kanuni na taratibu.


Pia, amewataka Wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wanapotendewa vibaya na watumishi hão ili hatua stahiki zichukuliwe.


Akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka kuhusu lini Serikali itatoa vibali vya Uwindaji, amesema Vibali vya uwindaji wa kitalii vinaendelea kutolewa kwa mujibu wa Kanuni husika ambapo hadi sasa jumla ya minada saba (7) imefanyika na wadau wamepewa vibali vyao.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »