SERIKALI YAZINDUA MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA NA USALAMA WA CHAKULA NCHINI

SERIKALI YAZINDUA MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA MIMEA NA USALAMA WA CHAKULA NCHINI

Na Barnabas Kisengi-Dodoma Katika swala la kuimarisha usalama wa chakula nchini serikali imezindua mradi wa miaka mitatu na miezi sita wa uboreshaji huduma za afya ya mimea Tanzania utakaogharibu kiasi cha EURO milioni 10.1. Naibu waziri wa Kilimo Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa uboreshaji wa afya za mimea kuwa serikali  kupitia Wizara ya

Na Barnabas Kisengi-Dodoma


Katika swala la kuimarisha usalama wa chakula nchini serikali imezindua mradi wa miaka mitatu na miezi sita wa uboreshaji huduma za afya ya mimea Tanzania utakaogharibu kiasi cha EURO milioni 10.1.

Naibu waziri wa Kilimo Antony Mavunde amesema hayo katika uzinduzi wa uboreshaji wa afya za mimea kuwa serikali  kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliingia mkataba wa kutekeleza mradi wa Kuimarisha Afya ya Mimea na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU).

Mradi huu wa miaka mitatu na miezi sita unafadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mfuko wake wa Maendeleoa (EDF), Shirika la Umoja w a Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO) na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Mavunde amesema FAO ni wasimamizi wa mradi na utekelezaji hufanywa na serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viutilifu (TPHPA) iliyo chini ya Wizara ya Kilimo.

Aidha Mavunde amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa bajeti ya jumla EURO Milioni 10.1 ikiwa ni mashirikiano ya ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EUR Milioni 9.5), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula – FAO (EUR 350,000) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (EUR 250,000).

Mavunde amesema mradi huo unalenga kuhakikisha usalama wa chakula nchini kwa kuimarisha mfumo wa ukaguzi na utoaji wa vyeti vya usafi wa mazao yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi.

Pia mradi huo unalenga kudhibiti visumbufu vigeni kwa kuhakikisha mazao yanayoingia au kutoka nchini yana ubora unaokidhi viwango vya masoko ya kimataifa.

“Nachukua fursa hii kuwashukuru Umoja wa Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula (FAO) kwa kufadhili na kusimamia fedha za mradi huu muhimu. Ni imani yetu kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa na hivyo kuongeza upatikanaji wa masoko ya kimataifa na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na wa mtu mmoja mmoja”amesisitiza Mavunde.

Vile vile amesema mradi huo ulitokana na ukaguzi uliofanyika hapa nchini mwaka 2017, katika mifumo maalum ya udhibiti wa mimea na mazao yanayosafirishwa kwenda nchi za Umoja wa Jumuiya ya Ulaya.

“Ukaguzi ulibaini mapungufu yalikuwa sehemu ya Afya ya Mimea katika maeneo yafuatayo, maarifa madogo kwa wakaguzi wa afya ya mimea kuhusu matakwa ya usafi wa mazao na bidhaa za kilimo zinazoingizwa katika nchi za Umoja wa Ulaya,kukosekana kwa mfumo wa kufanya kukusanya takwimu za visumbufu vya mazao,kukosekana kwa maabara maalum zenye uwezo wa kufanya uchunguzi muhimu ili kuthibitisha cheti cha usafi wa mimea kinachotolewa kwa mimea na mazao yanayokidhi vigezo na masharti ili kufikia masoko ya kimataifa,.

“Kutokuwepo kwa utaratibu wa kutambua masuala ya usafi wa mimea na maarifa madogo kuhusu matakwa yaliyopo ya ubora wa mimea na mazao wakati wa usafirishaji kufikia soko husika”amesema Mavunde

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viwatilifu Tanzania(TPHPA), Dk. Efraim Njau, alisema sekta ya kilimo ni muhimu sana ambapo imeajiri zaidi ya asilimia 67 ya watanzania na kuchangia takribani asilimia 29 ya pato la taifa.

 “Matokeo tarajiwa ya mradi huu ni kuziongezea uwezo maabara za mamlaka kujenga, kukarabati na kuweka vifaa katika maabara za Mamlaka, kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa visumbufu na masalia ya viuatilifu katika mnyroro wa thamani ya uzalishaji wa mazao hususan ni yale mbogamboga na matunda,” amesema Njau

Mwakilishi wa FAO, Nyebenyi Tipo, alisema mradi huo umelenga kuhakikisha usalama wa chakula hasa kwa mazao yanayovuka mipaka kwa kuhakikisha yanakuwa na ubora.

xxxxxxxxxxxxxxx

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Kamati  ya Kudumu  ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma ,akitoa salamu za Kamati yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU Bw.Cedric Merel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bi. Nyebenyi Tipo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viwatilifu Tanzania  TPHPA Dkt. Efraim Njau,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akizindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa kuimarisha huduma za Afya ya Mimea na usalama wa Chakula nchini hafla iliyofanyika leo Septemba 21,2022 jijini Dodoma.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »