WAZIRI MASAUNI AONGOZA MAADHIMISHO YA 92 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI MASAUNI AONGOZA MAADHIMISHO YA 92 YA SIKU YA TAIFA LA SAUDI ARABIA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022. Mhandisi Masauni alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Balozi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022. Mhandisi Masauni alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ali Alsheryan.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Balozi Abdullah Ali Alsheryan (watatu kulia) pamoja na Afisa wa Ubalozi huo, wakikata keki ya maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza. Masauni alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulshoto ni Balozi wa taifa hilo nchini Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Balozi Abdullah Ali Alsheryan (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza (kushoto) na Afisa wa Ubalozi huo (kulia), wakipongezana baada ya kukata keki ya maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Balozi Abdullah Ali Alsheryan (katikati), na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camilius Wambura, wakitoa heshima wakati ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa la Saudi Arabia katika maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa hilo yaliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022. Masauni alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya 

……………………………………………

Na Felix Mwagara, MoHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameipongeza Serikali ya Saudia Arabia kwa maadhimisho ya siku ya 92 ya Taifa hilo la Kifalme yaliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam, jana Septemba 22, 2022.

Waziri Masauni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya maadhimisho hayo, alisema Serikali ya Tanzania inatoa pongezi hizo kwa taifa hilo na pia kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha Uongozi wa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa pongezi kwa maadhimisho haya na pia inaishukuru Serikali ya Saudia kwa ushirikiano wa muda mrefu uliodumishwa kupitia sekta za kilimo, afya na maji na imeahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa faida ya nchi zote mbili,” alisema Masauni.

Waziri Masauni kupitia maadhimisho hayo amewakaribisha wawekezaji kutoka Saudia Arabia kuja nchini kuwekeza na pia kwa waliopo waendelee kuongeza nguvu zaidi ya kuwekeza kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyoboreshwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Balozi wa Saudi Arabia nchini, Balozi Abdullah Ali Alsheryan, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano waliokuwa nao kwa Taifa hilo na ameahidi wataendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »