TAKRIBANI WATOTO 800 HUGUNDULIKA NA SARATANI KILA MWAKA NCHINI TANZANIA

TAKRIBANI WATOTO 800 HUGUNDULIKA NA SARATANI KILA MWAKA NCHINI TANZANIA

Kutoka New York, Marekani Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  Septemba 23, 2022 ameweka wazi kuwa, kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania hivyo kuchangia ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa huo. Waziri Ummy amesema hayo katika kikao  na Taasisi ya Global HOPE iliyoko Texas nchini Marekani katika mkutano wa

Kutoka New York, Marekani


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  Septemba 23, 2022 ameweka wazi kuwa, kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania hivyo kuchangia ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.


Waziri Ummy amesema hayo katika kikao  na Taasisi ya Global HOPE iliyoko Texas nchini Marekani katika mkutano wa pembezoni baada ya Mkutano Mkuu wa 77 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea New York, nchini Marekani.
“Kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania, lakini kama Serikali tumeendelea kuboresha matibabu ya Saratani kwa watoto ili kuokoa maisha yao.” Amesema Waziri. Ummy.


Aidha Waziri Ummy asema kuwa, inakadiriwa kuwa watoto wenye saratani wanaoendelea kuishi zaidi ya miaka miwili kuanzia kugundulika ni kati ya 20% hadi 40%, huku katika nchi zilizoendelea ni zaidi ya 80%, hii ni kutokana na  kuchelewa kufanya uchunguzi, *kuasi* matibabu,  gharama za usafiri na malazi,  uchache wa vituo vinavyofanya uchunguzi na uhaba wa watumishi wenye ujuzi.


Waziri Ummy ameshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Hope Dkt. David Poplack Kwa msaada wanaoipatia Serikali ya Tanzania ambapo wanaoendelea kufadhili programu na kuwajengea uwezo watumishi hususan katika fani za ubingwa bobezi wa matibabu ya Saratani na magonjwa ya damu zaidi ya 10, na kutoa vifaa vya uchunguzi katika hospitali ya Muhimbili.


Sambamba na hilo, Waziri Ummy ameiomba Taasisi hiyo kuongeza idadi ya watanzania wanaopatiwa ufadhili wa mafunzo ya utoaji huduma za Saratani Kwa kada za Uuguzi, Madaktari ,Wafamasia na Wataalamu wa maabara.


Waziri Ummy amemwomba kujengea uwezo hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya katika kutoa huduma hizo Kwa kujenga na kuipatia vifaa vya kisasa vya huduma za Saratani.


Kwa upanda wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Hope Dkt.Polack amesema kuwa, Taasisi hiyo ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya kuimarisha huduma za Saratani nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »