KAMATI YA SIASA CCM KATA YA KILIMANI KUANDAA MKUTANO KUWASHUKURU WANACHAMA

KAMATI YA SIASA CCM KATA YA KILIMANI KUANDAA MKUTANO KUWASHUKURU WANACHAMA

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani imekutana katika kikao chake cha kwanza kwa mujibu wa Katiba kwaaajili ya kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo na kukijenga Chama cha Mapinduzi. Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Nathan Chibehe amesema “Sasa uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi kwa

Ña Barnabas Kisengi-Dodoma


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani imekutana katika kikao chake cha kwanza kwa mujibu wa Katiba kwaaajili ya kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo na kukijenga Chama cha Mapinduzi.

Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Nathan Chibehe amesema

“Sasa uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi kwa ngazi ya mashina, matawi na kata umekwisha hivyo ameomba makundi yaliyokuwa ndani ya Chama hicho kwa ngazi ya mashina, matawi na kata yavunjwe na kubaki na kundi la wana CCM tu ili kuendelea kukijenga Chama na kuingiza wanachama wapya”

Mwenyekiti amesema baada ya kumaliza chaguzi hizo, sasa Chama cha Mapinduzi kinaendelea na chaguzi za ndani ya Chama kwa ngazi ya Wilaya na wakimaliza wateendelea kwa nganzi ya Mkoa na kumalizia ngazi ya Taifa.

Aidha Mwenyekiti Chibehe amesema kamati ya Siasa ya kata inatarajia kufanya mikutano miwili mikubwa kwa tawi la Kilimani na tawi la Chinyoyo kwa lengo la kuwashukuru wanachama na pia kujitambulisha rasmi kwa viongozi waliochaguliwa hivi karibuni kukiongoza Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani.

Na baada ya kufanya mikutano hiyo ya kushukuru kamati ya Siasa itaanza kufanya ziara ya kutembelea matawi hayo mawili tawi la Chinyoyo na Kilimani kwa kusikiliza kero na changamoto kwa wananchi wa mtaa wa Chinyoyo na Image ili waweza kuziwakilisha Katika ngazi husika.

Lengo jingine ni kukagua mali na miradi ya chama katika matawi hayo mawili na pia amesema kamati ya siasa itaendelea kufanya ziara ya kukagua maeneo ya viwanja vya taasisi mbalimbali za kiserikali ikiwemo maeneo ya viwanja vya shule, zahanati, soko, kituo cha police na kiwanja cha ofisi ya CCM tawi la Chinyoyo.

Na baada ya kumaliza ziara hiyo ya kamati ya siasa ya kata watakuwa wamejua kero na Changamoto Mbalimbali kwa Wananchi na wanachama wa CCM wa kata ya Kilimani ambapo kama Chama wakiwa wanaisimamia Serikali watazifikisha eneo husika kwa kuzitatua au kuzimaliza kabisa na kusisitiza suaala la ulinzi na usalama wa kata ya Kilimani.

  

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »